ad

ad

HENRY ATIMULIWA MZUNGUKO MZIMA

IMEELEZWA kuwa, kiungo mkabaji wa Simba, Henry Joseph, atarejeshwa kwenye kikosi hicho katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Henry aliondolewa katika kikosi cha Simba hivi karibuni kutokana na kudaiwa kuonyesha utovu wa nidhamu, hasa baada ya kushindwa kufanya mazoezi ya Kocha Mkuu, Abdallah Kibadeni, akidai anaumwa.
 Henry Joseph.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya benchi la ufundi la timu hiyo, uongozi haumhitaji kwa hivi sasa na badala yake utamrejesha kwenye mzunguko wa pili.

Chanzo hicho kilisema, uongozi unaamini wachezaji waliopo kwenye kikosi hicho wana uwezo mkubwa wa kucheza nafasi yake.

“Uwezekano wa Henry kurejeshwa kikosini kwenye mzunguko huu wa ligi kuu ni mdogo kutokana na maamuzi yaliyotolewa na uongozi.
“Uongozi umepanga kumrejesha kikosini kwenye mzunguko wa pili wa ligi kuu, maamuzi hayo yametolewa baada ya kuwepo wachezaji wenye uwezo wa kucheza nafasi yake,” kilisema chanzo hicho.

Alipoulizwa Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala kuhusiana na taarifa hizo, alisema: “Hilo naomba aulizwe kocha aliyemsimamisha.”

Alipoulizwa Kibadeni akamtupia mzigo msemaji wa Simba, Ezekiel Kamwaga, ambaye simu yake ya mkononi ilikuwa ikiita bila kupokelewa.

Kiungo huyo alijiunga na timu hiyo katika usajili wa mwanzo wa msimu huu akitokea katika kikosi cha Kongsvinger cha Norway ambacho alikuwa amemaliza mkataba.
Powered by Blogger.