ad

ad

‘Kigogo wa madereva ameuawa kwa sumu’

 
Na Makongoro Oging’
YAMEIBUKA! Kifo cha Rashid Saleh ambaye ni Naibu Katibu Mkuu na Msemaji wa Chama cha Madereva Tanzania (Tadwu) kimeibua


mazito baada ya simulizi ya mjane wa marehemu, Fadhila Rashid kuonesha kuwa mumewe huyo alilishwa sumu iliyosababisha kifo chake, Uwazi lina cha kushika mkononi.
UWAZI NYUMBANI KWA MAREHEMU
Jumamosi iliyopita, siku moja baada ya kifo hicho, Uwazi lilifika nyumbani kwa marehemu, Kimara Baruti jijini Dar na kuzungumza na mke huyo maarufu kwa jina la mama Salma ambaye kwa upande wake, alidai kifo cha mumewe kilitokana na kulishwa sumu.
HAYA NDIYO MAELEZO YA MKE
“Nakumbuka ilikuwa Jumatano (Novemba 11, mwaka huu), asubuhi nilimwandalia mume wangu chai lakini hakunywa akadai amepigiwa simu na Mwenyekiti wa Muungano wa Vyama vya Madereva Tanzania, Clement Masanja, wakutane asubuhi hiyo waende kwenye kikao cha Chama cha Wamiliki wa Malori (Tatoa) kilichofanyika Hoteli ya Serena (Dar).
“Aliporudi nyumbani, mume wangu aliniambia yeye na Masanja baada ya kikao, walipitia nyumbani kwa mwanamke mmoja (jina lipo) ambapo walikaribishwa chai. Mume wangu alikunywa peke yake. Baadaye walipotoka walipitia baa moja iliyopo Ubungo, pale walikula ugali na nyama.”
IMG-20151122-WA0005HALI YAANZA KUWA MBAYA
“Mume wangu hali yake ilianza kuwa mbaya hapa nyumbani ambapo alilalamika kuumwa na tumbo. Ghafla akaanza kutapika na ‘kuendesha’. Awali tulifikiri ni kipindupindu, tukampeleka Zahanati ya Salama, baadaye Zahanati ya Arafa hapahapa Kimara ambapo walituambia tumkimbize Hospitali ya Palestina (Sinza) au Mwananyamala.
“Tulifanya hivyo, tukampeleka Palestina, akaongezewa maji zaidi ya chupa kumi. Alilazwa pale kwa siku tatu, akapata nafuu kidogo, tukamrudisha nyumbani.”
AKIMBIZWA KWA KAIRUKI
“Hata hivyo, hali ilibadilika tena, akaendelea kuumwa na tumbo kama awali, kutapika na kuendesha. Ikabidi tumpeleke Hospitali ya Kairuki (Mikocheni). Kule tuliwauliza madaktari kinachomsibu mume wangu ni nini, lakini hawakuwa wazi kusema.
“Hali ya mume wangu ilizidi kuwa mbaya jamani. Ilifika mahali akaniambia mke wangu, ‘kinachoniua ni nyama niliyokula’. Kila mara alikuwa akitamka hivyo, wale madaktari licha ya kunificha lakini mmoja wao alimwambia wifi yangu kuwa mume wangu amekula chakula chenye sumu. Basi, haikuchukua muda mrefu, mume wangu akakata kauli,” alisema mwanamke huyo na kuanza kulia.
KAULI YA MWISHO YA MAREHEMU
Baada ya kufuta machozi, mama Salma akaendelea: “Alipopata fahamu kauli yake ya mwisho alitaka aitiwe mtoto wake (Salma). Tulifanya hivyo. Salma alipofika hakumwambia kitu, alimkumbatia huku akitokwa machozi. Palepale nikaanza kutia shaka kwamba mume wangu anatuacha.
“Hali hiyo aliwalazimu madaktari kumchukua kwenye gari la wagonjwa na kumkimbiza Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Hiyo ilikuwa jana (Ijumaa iliyopita).
“Licha ya jitihada zote hizo, baada ya kupokelewa Muhimbili mume wangu hakuchukua muda akafariki dunia,” analia tena.
Akaendelea: “Mimi naamini kifo cha mume wangu si cha kawaida. Kuna namna kama alivyokuwa akilalamika marehemu. Naamini mume wangu ameuawa kwa kuwekewa sumu kwenye chakula.”
2.KaimuKatibuMkuuwaChamaChaMaderevaTanzaniaRashidSalehakihojiwanawanahabari.MWENYEKITI WA TADWU AONGEA
Naye Mwenyekiti wa Tadwu, Shaban Mdemu kwa upande wake, alisema amesikitishwa na kifo hicho huku akijiuliza ni kwa nini marehemu aliitwa kwenye kikao hicho cha Serena bila wito wa barua na kwa nini wao kama viongozi hawakuwa na taarifa rasmi ya kiofisi?
“Wakati tunamuuguza aliniambia mambo mengi juu ya mzunguko wake na alidai katika kikao hicho alipigiwa simu na mtu mmoja hivi.
“Marehemu aliniambia kuwa walihudhuria katika kikao hicho na Masanja na kupata kifungua kinywa kisha kwenda kula katika baa moja iliyopo Ubungo. Baadaye alirudi nyumbani na ndipo alipoanza kujisikia vibaya.
“Nilipigiwa simu, ikabidi niende kumchukua kwenda naye hospitali mbalimbali huku tukiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda. Hadi mauti yanamkuta Muhimbili tulikuwa na Makonda.
“Kusema kweli mkuu wa wilaya ameonesha ushirikiano mkubwa sana kwa kila hali na mali. Tunamshukuru sana.
“Lakini pia, kifo cha huyu ndugu yetu kimetuchanganya sana. Watu wengi wamekuwa wakidai kuwa ni sumu. Lakini mimi nimekuwa nikiwatuliza wasubiri ripoti ya daktari maana haijatoka.
“Kabla ya mauti, marehemu alimwambia mkewe kuwa amelishwa sumu na ndiyo inayomuua. Sisi viongozi tunataka majibu ya madaktari yaliyo sahihi baada ya hapo tutatoa tamko,” alisema Mdemu.
Bwana Rashidi SaleheMASANJA NAYE
Kwa upande wake, Masanja ambaye alikuwa naye katika kikao cha wamiliki wa magari naye alipotafutwa na Uwazi alisimulia kama ifuatavyo:
“Siku ya kikao nilipigiwa simu asubuhi na marehemu kwamba, twende naye kule Serena. Mimi nikakubali. Tulipofika tulipata kifungua kinywa na kikao kikaendelea.
lipofika saa 6:30 tukatawanyika. Mimi na marehemu tukapitia baa moja iliyopo Ubungo River Side kupata chakula cha mchana. Marehemu aliagiza mishikaki mitano na ugali, mimi nikaagiza nyama ya mbuzi na ugali.
“Baada ya hapo tuliondoka kila mmoja akaenda kwake mpaka niliposikia anaumwa ghafla na akapelekwa hospitali na siku chache baadaye mauti yakamkuta. Lakini nilikuwa nafika hospitali,” alisema Masanja.
Marehemu alisafirishwa juzi (Jumapili) kuelekea Kayenza, Mwanza na alitarajiwa kuzikwa jana (Jumatatu).
Powered by Blogger.