Bella kufunga mwaka na Koffi, Dar Live
KING of the Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’.
Na Mwandishi Wetu
KING of the Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’ anatarajiwa kufunga mwaka (Desemba 31) na wimbo alioufanya na mkongwe wa muziki kutoka Kongo (DRC), Koffi Olomide uitwao Acha Kabisa, ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.
Akizungumza na mtandao huu, Bella anayetamba na Wimbo wa Nashindwa alisema usiku huo mashabiki watafunga mwaka kwa kuimba na kucheza ngoma zake zote kali kama vile Nani Kama Mama, Nakuhitaji, Msaliti, Nashindwa, Amerudi na nyingine kibao.
“Usiku huo nitafunga mwaka na kufungua mwaka mwingine nikiwa na bendi yangu ya Malaika Music huku tukitoa sapraiz kwa mashabiki wetu wote, pia kwa mara ya kwanza nitawaonjesha Wimbo wa Acha Kabisa niliofanya na Koffi Olomide pamoja na kutambulisha wimbo wangu mpya mwingine,” alisema Bella.
Mashabiki pia wategemee kupata sebene la aina yake kutoka kwa Malaika itakayokuwa na vichwa kama Adaya, Petit Mauzo, Pilu, Mico Bella, Chesco Vuvuzela, Yanick Soslo, Babu Bomba, Kadogoo Machine na wengine wengine wengi.
Baada ya kufunga mwaka, katika Sikukuu ya Mwaka Mpya (Januari 1), bendi kongwe ya muziki wa Dansi, The African Stars ‘Twanga Pepeta’ ikiongozwa na Ali Chocky itakuwa na kazi moja ya kulishambulia jukwaa kwa kutoa sebene la kisasa. Akizungumzia shoo ya kufungua mwaka, Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo alisema kuwa siku hiyo pazia la burudani litafunguliwa mapema kuanzia asubuhi kwa kutoa nafasi kwa watoto wote kusherehekea kuukaribisha mwaka mpya. “Tutakuwa na kundi linalotikisa kunako miondoko ya sarakasi na mazingaombwe kwa watoto la Masai Warriors ambapo watatoa burudani zote bila kusahau watoto wote wataburudika na michezo mingi kama vile kuogelea, kuteleza, kubembea pamoja na kucheza ndani ya ndege maalum,” alisema Mbizo.
Post a Comment