BARCELONA YAIFUNZA ADABU MADRID, YAITANDIKA BAO 4-0
Barcelona
imeitwanga Real Madrid kwa mabao 4-0 licha ya kuwa nyumbani kwake Santiago Bernabeu.
Luis
Suare amepiga mabao mawili, Neymar akapiga moja na mkongwe Adres Iniesta naye
akapiga moja.
Hata
kabla ya Lionel Messi kuingia, Barcelona waliutawala mchezo kwa kiwango kikubwa
tokea kipindi cha kwanza.
Madrid
iliyokuwa ikipewa matumaini na mashabiki wake, huku wakiamini itafanya
marekebisho katika kipindi cha pili, ilizidi kuboronga.
Isco
naye akalambwa kadi nyekundu baada ya kumtandika teke la nyuma Neymar upande wa
goti.
Madrid ingeweza kufunga mabao angalau mawili au matatu kupitia Ronaldo, Benzema na Marcelo lakini hata hivyo ilikuwa kazi nzuri ya kipa Bravo wa Barcelona aliyefanya kazi nzuri sana kuokoa.

Post a Comment