Tamasha la Jokate latikisa Sekondari ya Jangwani, Dar
Mo Music akifanya yake jukwaani wakati watamasha hilo.
MWANAMITINDO maarufu nchini na mmiliki wa kampuni ya Kidoti
Foundation, Jokate Mwegelo maarufu kwa jina la Kidoti amefanya tamasha
kubwa katika shule ya sekondari Jangwani, jijini Dar es Salaam, tamasha
ambalo limehudhuriwa na wanafunzi kutoka shule mbalimbali za jijini Dar
es Salaam ikiwemo Jangwani, Azania, Makongo na nyingine.
Lengo kuu la tamasha hilo ilikuwa ni
kuhamasisha wanafunzi katika vipaji mbalimbali ambapo walipewa fursa ya
kuonesha vipaji vyao kwa kufanya shoo ya kuimba, kucheza na michezo
mbalimbali na kuonesha mitindo.
Wasanii waliotumbuiza kwenye tmasha hilo ni Ally Kiba, Niki wa Pili, Pamera Daffa ‘Pam D’, Mo Music na Ruby.Mbunifu wa mavazi, Martin Kadinda alipata fursa ya kuwazawadia wanafunzi walioweza kuonesha vipaji vyao, kiasi cha Tsh. 50,000/= kila mmoja kwa niaba yaw engine.
Pesa zilizopatikana kutokana na kiingilio kwenye ntamasha hilo zitaingizwa kwenye mfuko wa Kidoti Foundation kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wasichana wanaosoma katika mazingira magumu sehemu mbalimbali nchini.
PICHA NA MAYASA MARIWATA/GPL

Post a Comment