ad

ad

Dude achomoa ishu ya kumbadili dini kwa Ester Kiama!

Ester Kiama 

dude2.gif
STAA wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’, ameweka wazi kuwa kubadili dini kwa msanii anayetajwa kuwa mpenzi wake, Ester Kiama hakuhusiani na yeye kama watu wanavyodai.
Akipiga stori na paparazi wetu, Dude alidai kuwa kuna minong’ono mingi ya chini kwa chini kwamba anambadilisha Ester awe Muislamu kama yeye kitu ambacho si sahihi kwani suala la kubadili dini ni la mtu mwenyewe kuamua.

“Suala la imani ni la mtu binafsi kiukweli lakini inategemea na malezi aliyokuwa nayo huko nyuma, labda kaamua kufuata dini ya mama yake au wajomba zake kwa sababu kalelewa sana upande wa mama ambako chimbuko lao ni Uislamu,” alisema Dude.
Kwa kipindi kirefu wawili hao wamekuwa wakidaiwa kuwa ni wapenzi hadi kufikia hatua mke wa Dude kuondoka nyumbani kisha  baadaye kurejea na kupatana kwa masharti kwamba Dude apime Ukimwi ndipo waendelee suala ambalo mwigizaji huyo aliliafiki.

Habari na Shani Ramadhani wa Global Publishers
Powered by Blogger.