Lulu bado amtesa mama kanumba
MAMA
mzazi wa aliyekuwa staa wa filamu, marehemu Steven Kanumba, Flora
Mtegoa, bado anateswa na Elizabeth Michael kufuatia maandishi yake
kwenye mitandao ya kijamii katika siku ambayo ilikuwa ni kumbukumbu ya
kifo cha mwanaye.
Akipiga
stori na gazeti hili, Flora alisema alihuzunishwa na maneno aliyoandika
mpenzi huyo wa zamani wa mtoto wake kuwa hawezi tena kumlilia Kanumba,
bali watu walio muhimu kwake anaowaangalia kwa sasa ambao ni mama yake
mzazi na mdogo wake, hali iliyomfanya apate presha na kulazwa
hospitalini zaidi ya mara tano.
“Ukweli
nina uchungu na ninaumia sana, yaani imebaki stori, haiwezi kujirudia
tena kama zamani, niliumizwa sana na maneno yake mitandaoni, pia usiku
ule wa siku ya kifo cha Kanumba pale Serena Hoteli alifanya sherehe na
kuweka picha ya Dk. Cheni na Ali Kiba akisema ni watu muhimu kwake,”
alisema mama huyo.

Post a Comment