AZIZA WA FACEBOOK - 3

ILIPOISHIA
MIMI: Hahaha! Umeonaeee. Hakuna gharama kabisa. Ila poa, usijali. Ngoja nimtumie friend request halafu nianze kumfanyia uninja. Ila niandalie zawadi yangu.
SASA ENDELEA:
EDUADO: Usijali kaka. Wewe fanya yako, ukimaliza, niache nami nifanye yangu. Au sio?
MIMI: Poa. Mia mia. Ngoja nianze kazi.
EDUADO: Shwari. Ngoja nifanye yangu. Nataka nimfuate mtoto Magreth hapa.
MIMI: Ndio yupi huyo?
EDUADO: Si yule wa Facebook wa kipindi kileeeee.
MIMI: Kwani ushang’oa?
EDUADO: Chezea mimi wewe. Mimi noma…kama ni wembe basi Gilette.
MIMI: Sasa mbona hujamkata Aziza kama ni Gilette.
EDUADO: Aziza ana chembechembe za chuma. Ningemkataje? Huyo nakuachia kama wewe mwenye yale maji ya kuyeyushia vyuma ndiyo utaenda nae sawa.
MIMI: Basi poa. Acha nikufanyie kazi yako mkurugenzi. Kazi hii niliachana nayo zamani sana ila kwa ajili yako, navaa gwanda nikukamilishie halafu nisepetue.
EDUADO: Mia mia.
Hapo nikatulia kwanza. Nikaanza kujifikiria ni kwa jinsi gani nilitakiwa kuanza kumfuata msichana Aziza. Kitu ambacho kilikuwa kikiniumiza kichwa changu kwa wakati huo ni kwamba hata Aziza mwenyewe sikuwahi kumuona kwa hiyo niliogopa kuuziwa mbuzi kwenye kiroba kama ilivyokuwa kwa Sikitu. Ngoja nikupe kijistori changu na huyu Sikitu.
Eduado alinifuata inbox na kuniambia kuhusu Sikitu, alimsifia na kumpamba sana, alinifanya nivutiwe naye sana na yeye alitaka nimchukue, nikasema poa. Mzee nikaanza mishemishe zangu kama Michael Scorfield wa Prison Break na kweli ndani ya wiki mbili, mtoto akawa mikononi mwangu. Unajua jinsi mtu anavyokwambia kwamba msichana mzuri hata kama wewe mwenyewe haujamuona unaanza kumtengeneza msichana wako kichwani, hivyo ndivyo nilivyofanya kwa Sikitu.
Nikamtengeneza Sikitu wangu kichwani, kumbe nilikuwa namuumba Sikitu wa tofauti bila kujua. Siku aliponitumia picha yake inbox niione mara baada ya kumlazimisha sanaaa, akanitumia. Alikuwa mrembo lakini hakuwa na urembo kama ambao Eduado aliniambia. Nikaachana naye.
Sikitu hakukoma, chating zangu nzuri za inbox za maneno ya hapa na pale alikuwa akizipenda sana, hivyo alitaka tuendelee kuchati. Haikuwezekana tena, nilimkatia maguu mara baada ya kuniambia kwamba anaishi Musoma, mbaya zaidi huku Dar hakuwa hata na ndugu kwa hiyo hakuwa na ndoto za kuja Dar, sasa mimi ningeonana naye wapi? Yaani nisafiri mpaka Musoma kwa ajili yake? Niliona kuwa suala gumu sana kufanyika. Basi ndio hivyo, tukapotezana potezana na hatimaye mapenzi kutoweka, siku hizi simuoni, bila shaka, kaniblock.
Baada ya miezi miwili, leo Eduado kaja na mpya, kaja na mrembo mpya ambaye wala sijawahi kumuona, huyu anaitwa Aziza. Sikutaka kufanya vitu kwa presha sana, nilichokifanya ni kumuomba urafiki na kisha kuanza kusubiria majibu.
Kila siku nilipokuwa naingia Facebook, hakuwa amenikubalia, sikuwa na shaka, niliendelea kusubiria zaidi na zaidi na baada ya siku mbili, akakubali kuwa rafiki yangu, furaha iliyoje? Hapo ndipo nilipoamua kuuanza mchezo wangu, mchezo uleule ambao ulimfanya Sikitu kuchanganyikiwa kwangu, ila kwa hapa, kutokana na sifa ambazo niliambiwa na Eduado, ilinipasa nitumie mbinu kubwa zaidi, mbinu ambazo zingeendana na uzuri wake, mtoto wa Kipemba bwana, hakutakiwa kufuatwa kikawaida, nami nikaanza kumfuata Kipembapemba na mapenzi ya Kihindi….mtu mzima nikawa najiona kama Shahruk Khan vile.
***
Mtu mzima nikaingia kazini kwa ajili ya kuanza kazi yangu ambayo nilikuwa nimepewa ya kuhakikisha kwamba mtoto wa Kipemba, Aziza anakuwa wangu. Ni kweli kwa mambo ambayo alikuwa amenieleza Eduado yalikuwa yamekwishanitenga kwa kiasi kikubwa sana kutoka kwa Aziza lakini ilitakiwa pia nifanye yangu katika kipindi hicho.
Kitendo cha Aziza kuukubali urafiki pamoja nami kilionekana kuwa kitu kizuri sana, kwa hiyo nilichokifanya nikajifanya bonge la bwege, nikamfuata kwa wall yake na kuandika ‘Asante A’ na kisha kusikilizia.
Kweli, kama alivyosema Eduado ilikuwa vilevile, mrembo hakui-LIKE asante yangu wala kuitolea comment, nikaona poa, vyote hivi ni mwanzo wa kumbukumbu zangu nitakazompa hapo baadaye. Kwa upande wa Eduado, hakutaka kujishika, kila siku alikuwa akinisumbua tu kwa inbox.
EDUADO: Kaka vipi?
MIMI: Kuhusu nini?
EDUADO: Mtoto. Hujaniambia chochote kile. Umefanikiwa au?
MIMI: Wewe umeniambia mambo mengi kuhusiana na huyu mrembo, unadhani ningeweza kukamilisha ndani ya siku tatu?
EDUADO: Hapana. Nilikuwa nauliza manake nimeona hapa sasa hivi u rafiki yake.
MIMI: Yeah! Ni rafiki yangu ila kila kitu kinatakiwa kufanywa kimahesabu.
EDUADO: Usiniangushe basi Sharukh Khan.
MIMI: Hilo usijali.
Katika kipindi hicho nilikuwa nafikiria mambo mengi sana, huyu mtoto kwangu alionekana kuwa na pozi ajabu, yaani nilikuwa nikizipitia post za kizushi alizokuwa akiziweka, watu walikuwa wakicomment halafu yeye hatokei.
Itaendelea leo saa moja usiku
Post a Comment