Steve Nyerere akijaza jina lake kwenye daftari la wagombea ubunge kabla ya kukabidhiwa fomu.
Wasanii wa maigizo Bongo, Catherine Rupia 'Cathy' (katikati) pamoja na Ndumbagwe Misayo 'Thea' wakishudia uchukuaji fomu hiyo.
Steve Nyerere (kulia) akionesha fomu baada ya kukabidhiwa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi, Athuman Salum.
Katibu
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kinondoni, Athuman Salum Shesha
akiagalia kadi ya uanachama ya CCM ya Steve Nyerere.
Wakili
wa kujitegemea, Emmanuel Makene akisaini katika daftari la kuchukua
fomu wakati alipokuwa akiirudisha, anayeshudia kushoto kwake ni mkewe,
Salah Makene pamoja na wengine alioambatana nao.
Makene (katikati) akishikana mkono mara baada ya kumakabidhi Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Athuman Salum.
Steve
Nyerere akihojiwa na wanahabari baada ya kushuka katika gari lake
kwenye ofisi za Chama Cha Mapinduzi, Mkwajuni Kinondoni kwa ajili ya
kuchukua fomu.
Wawili
(katikati) ni mke na mume, Emmanuel Makene,Salah Makene pamoja na ndugu
wengine alioambatana nao wakiwa katika picha ya pamoja nje ya Ofisi za
Chama Cha Mapinduzi, Mkwajuni Kinondoni.
MSANII wa maigizo Bongo, Steven Mengere ‘Steve
Nyerere’ anatarajia kutifuana vilivyo na wakili wa kujitegemea ambaye
pia ni mjumbe wa kamati ya siasa Kinondoni, Emmanuel Makene kwenye
kinyanganyiro cha kugombea ubunge katika Jimbo la Kinondoni jijini Dar
es Salaam.
Steve, amechukua fomu ya kugombea kiti cha ubunge leo na kuijaza kisha kuirudisha tayari ikiwa imekwisha jazwa.
Wakati akichukua fomu ya kugombea ubunge, Steve alisema haoni sababu ya
kiongozi bora kuchukua fomu na kukaa nayo zaidi ya siku mbili hivyo huo
ni uzembe kwani yeye amechukua na kurejesha papo hapo.
Hata hivyo, katika uchukuaji fomu hizo alijitokeza wakili wa
kujitegemea ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Kinondoni,
Emmanuel Makene ambaye naye anatarajia kugombea katika Jimbo la Wilaya
ya Kinondoni.
Post a Comment