MAN CITY YATUPWA NJE UEFA
Barcelona imefanikiwa kufuzu hatua ya Robo
Fainali ya Kombe la Mabingwa Ulaya kwa kuifunga Manchester City bao 1-0
lililofungwa na Ivan Rakitic dakika ya 31 ya mchezo uliopigwa Nou Camp,
Barcelona usiku huu na kuitupa nje City kwa jumla ya mabao 3-1.
Katika mechi ya kwanza iliyopigwa Etihad nchini England, Manchester City walilala kwa mabao 2-1.Katika mchezo mwingine wa michuano hiyo, straika wa Juventus, Carlos Tevez aliifungia timu yake mabao 2 dakika ya 3 na 79 wakati ikiichapa Borussia Dortmund kwa mabao 3-0 huku bao lingine likiwekwa kimiani na Alvaro Morata dakika ya 70.
Kwa matokeo hayo, Juventus nao wamefuzu hatua ya robo fainali huku Dortmund wakifunga virago.
Post a Comment