WAZIRI SITA AMSIMAMISHA MKURUGENZI MAMALAKA YA BANDARI
Waziri wa Uchukuzi, Samwel Sitta.
Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Bandarini aliyesimamishwa kazi Maden Kipande.
HABARI zilizotufikia muda huu zinasema Waziri wa Uchukuzi, Samwel
Siita, amemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari
nchini, Madeni Kipande, kutokana na matumizi mabaya ya ofisi
yaliyoisababishia serikali hasara ya mabilioni ya shilingi.Kusimamishwa kwa Kipande kunatokana na vyombo vya habari kufichua ufisadi uliokuwa unafanywa na mkurugenzi huyo ikiwa ni pamoja na kuwasimamisha wafanyakazi kinyume na taratibu na sheria.
Kashfa nyingine inayomsakama Kipande ni kuruhusu watu waliosimamishwa kazi bandarini kwa zaidi ya miaka miwili kuendelea kupokea mishahara na marupurupu kama kawaida.
Post a Comment