BELA AMSHANGAA KARAMA KUMKUMBUKA!
MSANII wa filamu na muziki, Isabela Mpanda Bela amemshangaa msanii mwenzake ambaye pia alikuwa mchumba wake, Luteni Karama kwa kumkumbuka siku ya wapendanao Valentines Day.
Msanii wa filamu na muziki, Isabela Mpanda Bela.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Karama aliweka picha ya Bela kisha akaambatanisha na maneno yaliyosomeka;
Najua kuna mengi yanatuvuruga na hiki kikwazo cha sasa, ila jua wewe ndiye Valentine wangu, sijui kwa upande wako.
Baada ya kunyaka ujumbe huo wa hisia za kimapenzi, paparazi wetu alimvutia waya Bela kujua kama ndiyo wamerudiana.
Aliyekuwa mchumba wa Bela, Luteni Karama.
Sipo naye, huo ujumbe wake nimeuona na nimemshangaa sana, ila sina cha kumjibu ndiyo maana nimekaa kimya, alisema Bela.
Bela na Karama walidumu katika uhusiano kwa muda mrefu na kuripotiwa kutaka kuoana mwishoni mwa mwaka jana. Mwanzoni mwa mwaka huu waliachana huku Bela akionyesha mahaba niue kwa Kiserengeti Boy kinachoitwa Dogo Nasri.
Post a Comment