BUNGE LAAHIRISHWA BAADA YA VURUGU KUHUSU POLISI KUWASHAMBULIA WAFUASI WA CUF
Mbunge wa NCCR–Mageuzi, James Mbatia.
Baada ya James Francis Mbatia kuleta hoja ya dharura juu nguvu
iliyotumiwa na polisi dhidi ya maandamano ya CUF jana, ili ijadiliwe na
wabunge kama hoja ya dharura, Spika Makinda aliamuru serikali ilete
majibu kesho ndipo ijadiliwe.
Spika wa Bunge, Anne Makinda, akiongozwa na mpambe kuingia kwenye ukumbi wa Bunge.
Wabunge walisimama kushinikiza hoja ijadiliwe lakini Makinda
aliendelea na msimamo wake wa hoja kujadiliwa kesho baada ya serikali
kuleta majibu. Hapo ndipo sintofahamu ilipozidi na kuleta kutoelewana
kati ya wabunge wa upinzani na spika na Ilibidi spika aahirishe bunge
mpaka kesho lakini baadaye akabadili na kusema litarejea saa kumi jioni
leo.
Post a Comment