BEKI MPYA SIMBA AZUA BALAA ZANZIBAR
BEKI mpya wa Simba, Hassan Kessy amezua balaa kisiwani hapa baada ya kumchezea rafu mbaya kiungo wa Mtibwa Sugar, Ibrahimu Rajabu, ‘Jeba’ wakati timu hizo ziliposhuka uwanjani juzi usiku kuwania Kombe la Mapinduzi kwenye Uwanja wa Amaan.

Viongozi wa Mtibwa Sugar wamekipokea kitendo hicho kwa jicho baya kwa kuwa Kessy alijiunga na Simba hivi karibuni akitokea kwa Wakata Miwa hao.
Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Mecky Maxime ameliambia Championi Jumamosi kuwa kitendo hicho kilichoonyeshwa na beki huyo ambaye amemlea mwenyewe si cha kiungwana hata kidogo.
“Inawezekana ndivyo alivyotumwa na kocha wake, lakini kusema kweli jambo hilo limenisikitisha sana na si la kiungwana kufanywa na mchezaji kama yeye ambaye nimemlea mwenyewe, lakini sina chuki naye,” alisema Maxime.

Post a Comment