EMMANUEL OKWI ANASAKWA KWA RB DAR
ANASAKWA kwa nguvu kubwa kama vile ambavyo mtuhumiwa wa kesi ambaye amefunguliwa jalada kituo cha polisi na kutolewa hati ya kusakwa na kutiwa nguvuni (RB) inavyokuwa.Ndivyo viongozi wa Simba walivyoanza kufanya msako wa nguvu wa kumtafuta kiungo mshambuliaji wa timu hiyo asiyeishiwa na vituko Mganda, Emmanuel Arnold Okwi.
Hiyo ni siku chache tangu uongozi wa timu hiyo kupata taarifa za kiungo huyo kuwepo jijini Dar es Salaam ‘akiponda raha’ huku timu yake ikiwa Zanzibar ikishiriki Kombe la Mapinduzi.Awali, taarifa zizokuwepo zinasema kuwa kiungo huyo alipewa ruhusa na viongozi wake kurudi kwao kwa ajili ya kwenda kumalizia fungate, kutokana na kufunga ndoa hivi karibuni.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya uongozi wa timu hiyo, zipo taarifa za kiungo huyo kuwepo nchini, hivyo viongozi wanafanya juhudi za kumsaka kwenye maeneo yote ya Jiji la Dar.
Chanzo hicho kiliongeza kuwa, viongozi wenyewe ndiyo wanaosababisha kiungo huyo kuisumbua timu kutokana na jinsi wanavyomlea tofauti na wachezaji wengine.
Kiliongeza kuwa, kabla ya kiungo huyo kusaini alionyesha nidhamu kubwa kwenye timu ikiwemo kuripoti mapema kambini na kujibidiisha uwanjani, lakini baada ya kusaini akabadilika na kuanza kurudia tabia yake ya mwanzoni.
“Hivi ni kweli Okwi yupo Dar? Kama kweli yupo basi atakuwa mchezaji wa ajabu kwa kweli, kwa sababu haiwezekani yeye awe Dar wakati ameomba ruhusa ya kurudi kwao kwa ajili ya mambo ya kifamilia.
“Inavyoonekana alikuwa anaficha makucha kwa viongozi ili tumuongezee mkataba, kwa sababu kabla ya kuongeza mkataba alikuwa anawahi kambini na kujibidiisha uwanjani, ghafla tunamshangaa amebadilika, simu zake zote hazipatikani,” alihoji kiongozi huyo.
Alipotafutwa Katibu Mkuu wa Simba, Stephene Ally kuhusiana na hilo alisema “Mimi sina taarifa zozote za Okwi kuwepo hapa nchini, sisi tunachojua yupo Uganda.“Tunaendelea kufanya uchunguzi kuhusiana na hilo, tutakapopata ukweli uongozi utajua la kufanya japokuwa pia tumeshazisikia habari kuwa anaonekana Dar,” alisema katibu huyo.
CHANZO: CHAMPIONI
Mshambuliaji wa Simba, Mganda, Emmanuel Arnold Okwi.

Post a Comment