SEMINA YA FURSA YAWAONYESHA NJIA WAKAZI WA DODOMA
Mkurugenzi
wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group, Ruge Mutahabaakiongea na
baaddhi ya wakazi wa Dodoma mjini waliyohudhuria kwenye Semina ya Kamata
Fursa ndani ya Ukumbi wa Royal Villege mapema leo,ambapo aliweze
kuongea nao na kuwapatia mbinu mbalimbali za kujikwamua kupitia
lasilimali zilizopo kwenye mazo yapatikanayo ndani ya mkoa huo.
Msemaji
kutoka G5 One, Pius Mikongoti akiwalezea wakazi wa Dodoma namna ya
kunufaika kupitia huduma zitolewazo na GS One hasa katika kutumia
Barcode.
Msanii
wa kughani Mashairi, Mrisho Mpoto naye akijaribu kuwapa historia yake
ya mafanikio na namna alivyoweza kutumia fursa hadi kufikia hapo alipo
kwa sasa.
Afisa
Utekelezaji na mipango wa NSSF, Ally Mkulemba akitoa semina kwa wakazi
wa Dodoma huku akiwapa mbinu za kutumia fursa katika kusongesha
mafanikio kupitia mikopo mbalimbali itolewayo na Shirika hilo mapema leo
ndani ya Ukumbi wa Royal Villege.
Mrisho
Mpoto akimkabidhi kifaa cha kupimia magari mmoja wakazi wa Dodoma
Beatrice Chilewa (kulia), muda mfupi baada ya kujishindia moja ya swali
lililoulizwa na msemaji wa GS One Pius Mikongoti, ambalo lilikuwa
likimtaka ataje nchi tatu za Kusini mwa Jangwa la Sahara zinazotoa
Barcode na namba za utambulisho wa nchi hizo, wa kwanza kutoka kushoto
ni Mkurugenzi wa kampuni ya Josekazi Auto Garage ambaye ndiye mimiliki
wa kifaa hicho cha kupimia magari.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Josekazi Auto Garage, Joseph Mgaya akiwaeleza wakazi wa
Dodoma namna alivyotumia fursa na kumnya aweze kumiliki kampuni hiyo
inayojishugurisha na huduma za kutengeneza A/C za magari na Ndege na
nanamna alivyo wekeza hadi leo anakifaa kinachoweza kupima magari yote
na kujua matizo yote kwa halaka.
Baadhi
ya wakazi wa Dodoma waliyojitokeza kusikiliza mafunzo mbalimbali kwenye
Semina ya Kamata Fursa iliyokuwa ikifanyika ndani ya Ukumbi wa Royol
Villege.
Msanii
wa Bongo Fleva Mwasiti Almasi akijaribu kuwaonyesha wakazi wa Dodoma
namna alivyotumia Fursa iliyopo kwenye muziki na kufanikiwa kuwekeza
baadhi ya vitu kupitia mafao mbalimbali yatolewayo na Shirika la NSSF.
Sehemu ya watu waliyojitokeza kwenye Semina ya Kamata Fursa iliyokuwa ikifanyika ndani ya Ukumbi wa Royal Village.
Mmoja
wa wanasemina hao akiuliza swali lililotokana na mafunzo yaliyokuwa
yakitolewa na wasemaji mbalimbali wa Semina ya Kamata Fursa muda mfupi
kabla ya kumalizika kwa semina hiyo.
Mtangazaji wa Kipindi cha Leo tena, Gea Habib akizungumza jambo kwenye semina ya Kamata Fursa.
Meza kuu ya watoa mada ya Kamata Fursa wakijadiliana baadhi ya mambo yaliyokuwa yakiendelea mahali hapo.
Habari/Picha: Musa Mateja/ GPL/Dodoma

Post a Comment