DIDA: EZDEN AKIOA, NITAANZA KUMCHANGIA!
MTANGAZAJI mwenye maneno lukuki kutoka Radio Times
FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ amesema kuwa endapo mtalaka wake, Ezden
Jumanne akitaka kuoa yeye atakuwa wa kwanza kutoa mchango wa harusi
hiyo.
Mtangazaji kutoka Radio Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’.
Dida ambaye kwa sasa yupo singo, alisema
japokuwa wameacha na Ezden, lakini hana bifu naye kwa sababu anaamini
kuwa yuko katika harakati za kutafuta mke bora hivyo haoni shida
kumchangia.
Dida akiwa na mtalaka wake, Ezden Jumanne.
“Ninachoamini mimi Ezden bado anasaka mke mwema na hiyo ni nzuri na
wala siwezi kuwa na bifu na mtu wake yeyote atakayempata, nitapenda
sana. Haya ndiyo maisha yasiyokuwa na chuki yanayotakiwa,” alisema Dida.
Post a Comment