SIRI PENZI LA ANTI LULU, BONDI YAFICHUKA
Staa wa filamu Bongo, Lulu Semagongo ‘Anti Lulu’.
SIRI imefichuka juu ya wasanii wawili waliokuwa
wapenzi wa muda mrefu na kumwagana, Lulu Semagongo ‘Anti Lulu’ na Bondi
Sinan kwamba walipeana kiapo kizito, Ijumaa limetonywa.
Chanzo makini kilichoomba hifadhi ya jina lake kilidai kuwa, katika
mapenzi yao waliapizana kwamba hakuna ruhusa kwa mmoja wao kuzaa na mtu
mwingine na ndiyo maana wote walipokiuka, yaliwafika mazito.
“Kiapo ni kitu kibaya sana, hivi karibuni Bondi alifiwa na mwanaye na
Anti Lulu aliwahi kuwa na mimba ya mwanaume mwingine ikatoka,
ukiunganisha matukio unaona kiapo chao kinafanya kazi,” kilidai chanzo
hicho.
Baada ya kuzinyaka habari hizi paparazi wetu alimtafuta Anti Lulu
ambaye alifunguka: “Ni kweli tuliapizana lakini mwenzangu alikiuka na
kwenda kuzaa na mwanamke, mtoto amefariki na mimi nilibeba ujauzito
mimba ikatoka.
“Mimi na Bondi tumetoka mbali sana na naamini hawezi kumuoa mwanamke
mwingine zaidi yangu nikishamaliza mambo yangu na kuamua kutulia
nitarudi tu kwake na huyo Wastara atamuacha,” alisema Anti Lulu.
Post a Comment