MAINDA AMLILIA SHERRY MAGARI
Staa wa Filamu za Kibongo, Ruth Suka ‘Mainda’.
Akizungumza na Ijumaa juzi, Mainda alisema alikuwa amejipanga kwenda
kumuona jana ‘Alhamisi’ baada ya kusikia kwamba hali yake haikuwa nzuri
lakini ikawa imeshindikana kwani kabla ya safari alipata taarifa za kifo
chake.“Nimeumia sana tena sana, yaani dah! Amekwenda rafiki yangu, nilitamani sana kumuona akiwa hai tuongee lakini Mungu akaamua kutenda kazi yake,” alisema Mainda.
Marehemu Sherry Magari aliyefariki dunia hivi karibuni.
Sherry aliugua ugonjwa wa moyo kwa muda mrefu na kufikwa na mauti
alipokuwa amelazwa kwenye Hospitali ya Mkoa wa Morogoro. Mungu ailaze
roho yake mahali pema peponi. Amina.

Post a Comment