USIKU WA KIGODORO - 04
Endelea kulike: www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com
“Baby,” aliita Lina kwa sauti tamu sana ambayo kwa mwanaume yeyote rijali angevutwa nayo hata kama angeisikia kwenye simu tu.
“Yes dear,” alipokea James akiwa kwenye macho yaliyojaa ulegevu wa mahaba ingawa hakumshinda Lina ambaye alikuwa mbendembende.
“Nahisi naota.”
“Kwa nini baby?”
“Hivi kweli?”
“Kweli nini?”
“Nipo kitandani na wewe leo?”
“Hata mimi siamini Lina, wewe ni mwanamke niliyetokea kukupenda sana. Napenda ujivunie kwa hilo baby.”
“Asante dear jamani,” alisema Lina akiwa anamshikashika James sehemu ya mgongoni.
Mechi ilianza kwa Lina kumsoma James kwamba ni mwanaume wa namna gani, anayependa nini kwenye ‘uwanja’ na nini hapendi. Kwa hiyo alichokuwa akikifanya Lina na kufanya tukio halafu ‘kumsikilizia’ James kwamba ‘anariakti’ vipi!
Mfano, katika kugalagaza, Lina alipeleka mdomo wake kwenye sikio la kijana huyo na kumpumulia kwa nguvu, James akawa hoi.
Kumbe James naye alikuwa kama Lina. Kwa sababu ilikuwa ni mara ya kwanza kukutana kwenye mechi, Naye alijitahidi kusaka sehemu ambazo ni za msisimko kwa Lina. Alipeleka vidole kwenye kifua na kuzishika nido kwenye misumari yake ambapo Lina akawa kama amepoteza fahamu.
Kama vile hiyo haitoshi, James alipotoa mikono kwenye nido akavipeleka kwenye sehemu kuu na kumfanya Lina kuwa hoi bin taaban huku akisema maneno ambayo ili uyasikie ni lazima kulaza sikio kwenye kinywa chake…
“Baby tayari sasa,” James alimsikia akisema hayo baada ya kumsogelea kwa karibu ili kumsikiliza. James hakutaka kumsikiliza, akaamua kwenda mbele zaidi ambapo alipeleka vidole kwenye sehemu ya kukanyangia mguuni kwa Lina, kilio kikubwa kikasikika kutokea chumbani humo lakini kwa jinsi mlango na madirisha yalivyokuwa hata kama mtu angesimama kuemea mlango asingesikia kitu.
James alizidisha manjonjo kwa kumpapasa Lina sehemu ya nyuma ya magoti ambapo Lina alibaki ameduwaa, uwezo wa kusema lolote hakuwa nao tena.
James aliianzisha mechi kwa kupuliza filimbi uwanjani yeye mwenyewe, Lina akaipokea huku akimwimbia nyimbo mbalimbali za mahaba mpenzi wake huyo ilimradi mchezo uwe mzuri huku jasho likifichwa kwa kasi ya utulivu ndani ya uwanja.
Ni ndani ya dakika kumi tu, Lina akatangaza ushindi wake wa kwanza dhidi ya James huku akipokea mashambulizi ya piga nikupige bila kubutua.
Ndani ya dakika tano tena mbele, Lina akatangaza kupata ushindi mwingine wa pili huku James akiendelea kupeleka mashambulizi yenye kumpa ushindi mrembo huyo.
“Baby,” aliita Lina mara baada ya ushindi wa pili…
“Yes…”
“Upo vizuri darling.”
“Kweli?”
“Sana.”
Maneno ya Lina yalimsukuma James ambaye naye papo hapo akapata ushindi wake wa kwanza huku Lina baada ya kumsikia mwanaume wake akiwewesekea ushindi na yeye akaupata wa tatu wa bure kabisa.
Wote wakawa wanahema kwa kasi, hakuna aliyemsemesha mwenzake. Sanasana kuna wakati James alinyoosha mkono na kushika rimoti ya AC na kuongeza kidogo spidi ya kutoa baridi. Hapo, Lina alikuwa akimwangalia James kwa mbali kwa macho ambayo kama anayafumba lakini hajayafumba kabisa, unaweza kusema alikuwa akisinzia.
James alidondoka na kulala ubavuubavu akimwangalia Lina ambaye naye alipeleka mkono wake kwenye kiuno cha mpenzi wake huyo na kukishikashika kama moja ya mbwembwe ndani ya uwanja wa mapenzi.
Baadaye sana, wawili hao walirejea katika ungangari wao, walianza kuzungumza…
“Sweet,” aliita Lina kwa sauti ya chini sana…
“Yes,” James aliitika kwa sauti nzito.
“Nakupanda sana. Sijui itakuwaje?” alisema Lina huku James akiwa hajui nini maana ya kauli yake hiyo.
“Baby, kwa nini umesema hujui itakuwaje? Kwani si tumeshapanga kufunga ndoa au?”
“Ungejua niko kwenye ndoa mwenzako wala usingesema hivyo,” alisema moyoni Lina lakini kwa sauti akasema…
“Unajua siamini kama hiyo siku itafika dear.”
“Kwa nini isifike my love? Itafika tu, sisi kinachotakiwa ni kumwomba Mungu tu basi,” alisema kwa ujasiri mkubwa James.
***
Saa kumi na mbili, James alimwingiza Lina ndani ya gari kumrudisha nyumbani na si kazini kama alivyotoka. Ndani ya gari, kiyoyozi kilikuwa kwa kiwango cha juu huku Lina akifurahia maisha na kusema moyoni kwamba alipata mwanaume wa kweli na kulaani ni kwa nini aliwahi kuonana na mumewe, Semi na si James.
Lina alimwelekeza James na kuiegesha gari jirani kabisa na nyumbani kwake huku akimwambia…
“Kama nilivyokwambia dear, dada yangu ni noma sana baby, kwa hiyo nishushe hapa.”
“Oke. Lakini baby vumilia tu iko siku yatakwisha mke wangu. Tukifunga ndoa shemeji atatulia, ukali wote utaisha,” alisema James akimkazia macho Lina. Lina aliachia tabasamu laini lakini kila wakati alionesha kutaka kuendelea kuwa na James.
Ukweli ni kwamba, Lina aliamua kushuka pale ili kukwepa mtego wa kukutana na mumewe ambaye alijua akigundua hilo pangechimbika ile mbaya.
Wakati anashuka, Lina alimpa mdomo James, akaachia ulimi, ukapokelewa kwa kuvutwa kwa dakika kama moja nzima huku mrembo huyo akionesha kusisimka sana…
Mara, simu yake iliita, kuangalia namba ni mume wake…
“Haloo baby…”“Nahisi nimekupita ukiwa ndani ya gari upo na nani?”
“Ni rafiki yangu mbona, amekataa kufika nyumbani, ndiyo kageuza sasa hivi hapa,” alisema Lina huku akishuka kwenye gari hilo na kuanza kutembea bila kuagana na James ambaye alishikwa na mshangao.
James hakutaka kumuuliza kitu Lina, akaweka gia ya kurudi nyuma kisha akageuka na kuondoka. Lakini kichwani alipata tabu na kauli ndogo tu ya Lina ukiachilia mbali kule kuondoka. Nayo ni ile aliyoitoa wakati akipokea simu…
“Haloo baby…”
“Huyo baby ni nani? Ina maana Lina ana mwanaume mwingine? Haiwezekani…kama ni kweli nitatumia uwezo wangu wote nisambaratishe penzi lao,” alisema moyoni James huku akiingiza gari lake barabara kuu.
***
Lina aliendelea kuzungumza na mume wake kwa simu akijisafisha huku akikaribia nyumbani lakini alipomaliza ndipo akamkumbuka James na mazingira ya kuachana kwao muda mfupi uliopita…
“Haloo baby…”
“Daaa! Sasa pale si atakuwa ameshangaa, haloo baby, baby ndiyo nani wakati nilimwambia sina mpenzi tuliachana? Nimechemsha kweli. Nilichotakiwa kukifanya pale ni kutopokea simu ya mista,” alisema moyoni Lina, akajikuta akiumia sana.
Alisimama nje ya duka moja kabla hajafika nyumbani kwake, akampigia simu James…
“Lina,” James aliitika kwa sauti nzito…
“Baby nisamehe sana…”
“Kwani kulitokea nini Lina mpenzi?”
“Da! Yaani, unajua nini my love?”
“Ee…”
“Kuna yule jamaa yangu niliyekwambia tumeachana, ndiye aliyenipigia…”
“Sasa baby kama ni yeye, ndiyo uondoke bila kuniaga?”
“Unajua nini my love?”
“Sijui…”
“Alichonitendea, kila akipiga simu nahisi kukasirika.”
“Sasa kama ni hivyo, mbona ulivyopokea ulisema haloo baby?”
“Da! Ni mazoea yangu, mabaya sana. Napenda sana kusema baby hata kwa mwanaume ambaye si mpenzi wangu.”
“Basi uache tabia hiyo kuanza sasa, sawa Lina?”
“Sawa mpenzi wangu, nisamehe.”
“Poa, yameisha.”
“Nashukuru baby, sasa naingia ndani ukinitaka unitumie sms kama nilivyokwambia sista mnoko kweli, ananifanya mimi kama mtoto wake, tena wa chekechea.”
“Usijali d, ila na wewe ukiwa katika mazingira mazuri nipigie, sawa?”
“Sawa d.”
Lina alizama ndani kwake akiwa na amani baada ya kumaliza ishu nzito na James ambaye alimwita mchumba ingawa wakati mwingine alipokuwa amekaa mwenyewe alijiuliza nini hatima ya uhusiano wake huo.
***
Baada ya hapo, mapenzi yaliimarika zaidi na zaidi hadi ikafika hatua ya kukubaliana kuhusu ndoa ambapo vikao kwa James vilianza na Lina aliwahi kuhudhuria kama mara tano hivi.
Kwa upande wake, Lina aliweka kikao kwa ajili ya kitchen party tu ambapo alimtumia rafiki yake Agnes kumsimamia wakisingizia kwamba, hakuwa na ndugu jijini Dar.
Ndugu wa Agnes, kama mashangazi na rafiki zake wengine, akiwemo mama mkubwa walibeba jukumu la kusimamia sherehe hiyo mwanzo mwisho.
Siku ya kwenda kwenye sherehe ya kitchen party, Lina alimwomba ruhusa mume wake, Semi siku moja nyuma akimwambia kutakuwa na kitchen party ya rafiki yake.
Siku ya shughuli mumewe alimuuliza kisa cha kuondoka akiwa amebeba nguo kwenye begi badala ya kuvalia nyumbani, Lina alisema…
“Hili gauni nikilivalia nyumbani nitakuwa kituko mtaani, nitakwenda kuvalia kwa Eg…”
“Kwani lina nini hilo gauni?”
“Limeshonwa kwa madoido sana baby, linafaa kuvaliwa ukumbini tu.”
“Hebu tulione.”
Lina alisita kwanza akidai muda unakwenda, lakini akalitoa…
“Khaa! Sasa mbona gauni lenyewe limeshonwa kama wewe ndiye bi harusi mtarajiwa?”
“Hamna! Unajua wamealika ngoma ya kigodoro ndiyo maana magauni wamesema yawe hivi.”
“Oke poa.”
Lina aliondoka mpaka kwa Eg, akapokelewa kwa shangwe na ndugu wa Eg ambao walikuwa hawajui kama bi harusi huyo ni mke wa mtu tena kwa ndoa ya kanisani kabisa.
Akiwa kwa Eg, Lina alimpigia simu James…
“Baby, uko wapi?”
“Niko kwa Eg darling.”
“Kwa hiyo ndiyo kama hivyo, leo hatuonani siyo?”
“Hatuonani labda usiku sana maana si unajua kitchen party si ya wanaume baby?”
“Poa, kuna nini kimepungua?”
“Hakuna dear.”
Wakati mazungumzo yakiendelea, mume wa Lina alifunga breki nje ya nyumba ya Eg na kupiga honi ana shida na mke wake huyo…
“Pii pii piii!”
ITAENDELEA SIKU YA KEHOOOOO
Endelea kulike: www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com

Post a Comment