USIKU WA KIGODORO - 03
ILIPOISHIA:
Mume wa Lina, Semi alishtuka, akaangalia alipolala mkewe akagundua hayupo na ametoka na simu. Kwa mbali alimsikia akiongelea kutokea chooni, akaamka…
SASA JIACHIE…
ALITEMBEA kuelekea chooni lakini alikutana naye anatoka…
“Vipi, mbona kama unaongea na simu chooni?”
“Si mama Pendo huyo, saa zile naamka kuja chooni na yeye akapiga sasa nilibanwa na haja ikabidi nije huku naongea naye.”
“Anasemaje muda huu?”
“Anasema hajalala tumbo, nikiwa na nafasi asubuhi nimpeleke hospitali.”
“Shemeji naye, mbona hospitali ni karibu na kwake? Yaani we utoke huku mpaka kule halafu umchukue kurudi naye hospitali au yu mahututi?”
“Hamna, kwanza mpaka akuambie mwenyewe ndiyo utajua anaumwa, mimi mwenyewe sikujua mpaka aliponiambia.”
Kulipambazuka kabisa, Lina alijiandaa mumewe naye alijiandaa, wakatoka wote. Lina alishushwa nje ya ofisi yake mumewe akaendelea na safari.
Ile anakaa tu, Lina akashika simu kumpigia James…
“Baby…”
“Yes baby, niambie.”
“Nimeingia job baby.”
“Safi sana, mimi ulivyoniamsha nikaoga lakini sijatoka nyumbani.”
“Oke. Sasa baby nyumbani unaishi na nani?”
“Niko na wasaidizi wa kazi watatu.”
“Watatu wa nini wote hao?”
“Mmoja ni mwanamke mtu mzima, ndiyo huwa anapika na kufua. Wa pili wa kiume kijana, huyu anatunza mazingira na wa tatu ni mlinzi getini.”
“Du! Kweli baby unatakiwa kuoa sasa baby wangu.”
“Kha! Kwani unadhani ni kwa nini nilikuomba uwe mke wangu Lina? Kwanza nimekupenda, pili una sifa za kuwa mke. Wewe Lina ni wife material.”
Lina alicheka kidogo, akafurahi, akaendelea…
“Sasa unatoka saa ngapi?”
“Eee, kuna email nazisubiria kwa hapahapa nyumbani nataka kutuma mzigo Ufaransa kwa hiyo naseti mawasiliano.”
“Naweza kuja?” alisema Lina kwa kusitasita, moyoni aliamini James hawezi kukubali hilo la yeye kwenda kwake.
“Wao, karibu sana Lina, tena nitafurahi sana kukuona hapa kwangu.”
Lina hakuamini masikio yake, akashangaa na kumuuliza James…
“Kweli baby?”
“Yeah! Njoo, chukua teksi nitalipa mimi hapa.”
“Ni wapi?”
“Mbezi.”
Lina alikata simu, akaingia kwa mabosi wake na kuomba ruhusa ya dharura akaruhusiwa, akaondoka.
Alitembea kwa mwendo wa haraka hadi kituo cha teksi, akaingia kwenye mojawapo…
“Twende Mbezi Beach tafadhali.”
Safari ilianza huku Lina akiwa na mshawasha wa moyo, alikuwa na maswali kadhaa…
“Je, James akitaka kuduu na mimi?” alijiuliza mwenyewe.
“Mh! Kwa kweli kwa jinsi alivyonilaza na njaa jana sitakuwa na sababu, nitakubali tu. Maana mh! Hata hivyo, ni nafasi ya pekee ya mimi na yeye kukutana kimwili kwa mara ya kwanza tena nyumbani kwake.
“Ni heshima kubwa sana atakuwa amenipa, maana angekuwa mwanaume mwingine asingekubali kuniita kwake, angeweka kikwazo.”
Lina alipoingia Mbezi ya Tangi Bovu alimpigia simu James akapewa ramani halisi ya kufika kwake. Ilikuwa ramani rahisi sana kwani walifika hadi nje ya geti, honi ikapigwa, geti kubwa likafunguliwa.
“Umeambiwa ingiza gari ndani,” mlinzi alimwambia dereva akimchungulia kwa kutumia kioo cha dirisha.
“Sawa,” teksi ikaingizwa ndani, Lina akashuka.
Ile anashuka tu, James anatokea ndani kwa mlango mkubwa…
“My wife to be,” alisema James akiachia tabasamu pana huku mikono ameipanua tayari kwa kumkumbatia Lina…
“Yes Lina’s husband.”
Walikutana wakakumbatiana, Lina akamuwahi mabusu James kama matatu, naye akarudishiwa, wakaingia ndani huku James amemkumbatia Lina kwenye kiuno.
Lina alishangazwa sana na mazingira ya nyumba hiyo. Licha ya kuambiwa mlikuwa na watu watatu na mwenyewe James wa nne, lakini ilionekana kama wanaishi watu kumi na mbili.
Maana alipozama sebuleni tu, akatokea yule mwanamke, akamkaribisha Lina kwa adabu zote licha ya kwamba alikuwa mama mtu mzima, kabla hajatoka akatokea kijana mtunza mazingira huku mlinzi naye akiingia na boksi na kuliweka sehemu kisha akatoka.
Lina alishangazwa pia na ukubwa wa sebule kwani alikuwa kama yupo kwenye ‘nusu uwanja’ wa table tennis. Mbali na ukubwa huo alishangazwa na samani za ndani licha ya usasa wake lakini hizo hakuwahi kuziona tangu azaliwe.
“Enhee, za kazi baby?”
“Poa, vipi wewe?” aliitika Lina.
“Mimi mzima sana, namshukuru sana Mungu. Lakini namshukuru zaidi kwa kukuleta wewe hapa leo.”
“Mimi mwenyewe nimefurahi sana kwa kunikubalia kuja kwako leo,”
alisema Lina huku akipepesa macho sehemu mbalimbali za sebule hiyo, akampongeza James kwa kuwa na nyumba nzuri kama ile.
Baada ya salamu, James aliwaita wafanyakazi wake wote, wakafika na kukaa kwenye sofa, kila mmoja yake…
“Huyu anaitwa Lina, ni mtoto wa mzee Joseph Ambakucha pale Kijiji cha Kilole, Korogwe Tanga. We mama si umetokea Korogwe pia?” alihoji James akimwangalia mwanamke anayemsaidia kazi za ndani…
“Ndiyo, hapohapo Kilole. Na mzee Joseph Ambakucha namfahamu sana.”
Lina alimtumbulia macho, akahisi kama mwanamke huyo anaweza kuharibu mambo japokuwa yeye hakuwa anamkumbuka kwa sura…
“Na wewe mama umeishi pale?”
“Ee! Mimi nilikuwa naishi Mgandini, wengi wananijua kwa jina la mama Tabu, nyumba yangu iko jirani na ya mzee Hussein, yule ana watoto akina Sakina, Said, Mariam...”
“Ooo! Sakina, Said wote nawakumbuka. Lakini wewe sikukumbuki kabisa…”
“Si rahisi lakini dada zako, kaka zako nawajua. Namjua Kiliana, Josephine, Anna na Yonasi.”
Basi, baada ya hapo, James akaendelea…
“Huyu sasa ndiye mchumba wangu niliyewaambia nimempata mtu wa Korogwe, Tanga ndiyo huyu.”
“Lakini sasa mbona ana pete ya ndoa kwenye kidole?” alidakia yule mwanamke.
Kumbe siku hiyo Lina aliamua kuvaa pete bwana, akasahau kuivua wakati anakwenda nyumbani kwa James.
James alishtuka sana, Lina pia alishtuka lakini akajikaza asijulikane, kilishanuka…
“Mungu wangu…Mungu wangu,” alisema moyoni…
“Eti Lina! Ni nini hiyo mpenzi? Kumbe unanisaliti?”
“Hamna! Kwa sababu nyie hamtembei sana mitaani. Siku hizi wanawake wengi wanavaa pete za ndoa ili kukwepa usumbufu wa wanaume. Mwanaume akikuona una pete ya ndoa heshima inaongezeka kidogo…”
James alitazamana na yule mwanamke anayemsaidia kazi za ndani, mwanamke akasema…
“Hiyo ni kweli, hata mimi nakubaliana na wewe. Japokuwa kuna wanaume hawajali hata kama una pete ya ndoa lakini inasaidia kupunguza upungufu.”
“Ni kweli.”
James alikubaliana na hilo kwa kutingisha kichwa huku akimwangalia Lina kwa macho yaliyojaa mahaba mazito…
“Vipi baby?” aliita Lina akimwangalia James…
“Poa tu.”
Wakati huo wale wote walioitwa kutambulishwa walishaondoka. Walibaki wawili tu.
“Hapa ndiyo nyumbani kwako?”
“Yeah! Hapa ni nyumbani.”
“Da! Bonge la jumba. Ukisikia jumba la kifahari ndiyo hili.”
“Kweli Lina?”
“Sana tu, hongera sana bwana. Kwanza bado kijana mdogo lakini umejitahidi sana.”
“Asante baby, ndiyo maana nataka tufunge ndoa ili uje kuipamba nyumba hii.”
“Hilo tumwombe sana Mungu atupe afya na uzima.”
James alisimama na kwenda chumbani kwake, nyuma Lina akawa anashangaashangaa mapambo ya nyumba hiyo yalivyokuwa na mvuto.
Mara James alitokea. Moyoni aliamini ni siku mwafaka sana kwake kuivunja amri ya sita na Lina lakini alikuwa haamini kama atakubaliwa kwani msichana mwenyewe alitoka kazini na angerudi tena kazini…
“Labda mjaribu, akisema siku nyingine sawa,” sauti ilisema ndani ya moyo wa James.
“Baby sasa, si umechoka sana ukaoge upumzike kidoo kitandani, au?” alisema James huku akiangalia pembeni kwani alijaliwa kitu kinaitwa aibu.
“Poa. Lakini nikioga nitabadili nini sasa?”
“Kwani mpaka ubadili, si unavua hizo, unaoga unavaa taulo ukilala, ukiamka unaoga tena unavaa hizo unaondoka.”
“Poa.”
“Basi simama twende.”
Lina alisimama akatembea huku akiivua ile pete ya ndoa na kusema moyoni…
“Ilitaka kuniletea balaa bure, bahati njema nimepata mwanaume mwelewa.”
Aliingia kwenye chumba cha James na kukutana na vitu vya samani ambavyo hakuvitarajia. Kitanda cha kisasa, sofa moja kubwa, stuli ndogo mbili na kitu kama meza fupi sana kwa ajili ya kupandia kitandani.
Lina alishangaa kuona ndani ya chumba hicho kila kitu ni cheupe au kimechanganywa na rangi ya krimu. Mashuka meupe, pazia jeupe, kapeti krimu, foronya nyeupe, dari nyeupe, mlango hadi madirisha na makabati.
Kilichomshangaza sana Lina na kuona chumba hicho hakina choo na bafu kwa maana ya ‘master bedroom’ kama ambavyo alitarajia…
“Mh! Bonge la chumba, kila kitu kimehusika lakini amekosa kitu kimoja tu, choo cha ndani,” alisema moyoni Lina. Lakini moyoni alisifia chumba hicho kilivyo na nyumba nzima kwa ujumla kwamba ni ya kisasa.
“Sasa ukaoge my love,” alisema James. Lina akasimama na kupokea taulo kutoka kwenye mikono ya kijana huyo. Alichojoa nguo zake zote, akabaki kama alivyozaliwa kisha akajijaladia na taulo sasa, akawa anatembea kwenda mlango mkubwa…
“Bafu liko uani au?” aliuliza Lina…
“Oooh! Sorry, bafu lile pale,” James alimwelekeza Lina bafu ambapo kwa Lina alipoona mara ya kwanza alijua pana kioo kikubwa kumbe ni mlango wa kuingilia bafuni, alijisikia aibu kubwa kwa ushamba.
“He! Sikujua mpenzi wangu, samahani,” alisema Lina huku akimfuata James na kumkumbatia kisha akampiga mabusu mawili ya pande mbili za mashavu.
James alionesha kusisimkwa mwili, naye akamkumbatia, wakatazamana. Ilikuwa ni kitendo cha mara yao ya kwanza tangu waanze kufahamiana siku kadhaa nyuma.
Lina alisisimka sana, James pia. Walijikuta wakigandana na baadaye walipanda kitandani huku Lina akiwa ametupa taulo chini…
Endelea kulike: www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com

Post a Comment