NINI CHA KUFANYA MPENZI WAKO ANAPOWASILIANA NA EX WAKE?-2
Shukrani ziende kwake Muumba ambaye kwa mara nyingine ametupa nafasi
ya kukutana kwenye uwanja wetu huu, tukijuzana, kuelimishana na
kubadilishana mawazo kuhusu mambo mbalimbali yahusuyo uhusiano wa
kimapenzi.Wiki
iliyopita tulianza kuijadili mada hii kama inavyosomeka kwenye kichwa
cha habari kuhusu hatua unazopaswa kuzichukua unapogundua kuwa mpenzi
wako, mumeo au mkeo ana mawasiliano na mpenzi wake wa zamani (ex wake).
Tulianza na mfano halisi wa jinsi mwanamke mmoja aliyeishi na mumewe
kwa kipindi kirefu na kufanikiwa kupata watoto, alivyoumia baada ya
kugundua kuwa mumewe ana mawasiliano na mpenzi wake wa zamani kiasi cha
kutamani hata kuyakatisha maisha yake.
Niwashukuru wote waliochangia mada hiyo kwa ujumbe mfupi wa
maandishi, nilichokibaini ni kwamba tatizo linalomsumbua mwanamke huyo,
linawasumbua watu wengi sana lakini hawana pa kusemea.
Leo tunaendelea kuangalia dalili za hatari ambazo ukiziona kwa mwenzi wako, zinaashiria kwamba bado anampenda ex wake na kuna uwezekano mkubwa bado wanaendelea kuwasiliana. Tulianza na dalili ya kwanza ambayo ni mpenzi wako kumzungumzia ex wake mara kwa mara, iwe kwa mazuri au kwa mabaya.

2. Anazo namba zake za simu. Mapenzi yakishafika mwisho, namba ya
simu ya mliyeachana haina umuhimu tena lakini ukiona bado mpenzi wako
ameisevu namba ya ex wake kwenye simu yake au ameiandika kwenye diary,
hiyo ni dalili mbaya kwamba wanawasiliana. Endelea kuchunguza.
3. Anabadilika ghafla akimuona hata mkiwa pamoja. Yawezekana mpo
kwenye matembezi au shughuli za kawaida na mpenzi wako, ghafla ex wake
akapita mbele yenu na ghafla mwenzako akabadilika.
Mapigo ya moyo yakaanza kumuenda mbio, akakuachia mkono hata kama mlikuwa mmeshikana kimahaba, akatangulia mbele, kubaki nyuma au akamgeukia ex wake, hiyo ni dalili kwamba bado anampenda na kuna uwezekano mkubwa wakawa wanaendelea kuwasiliana.

4. Anajifanya ni rafiki yake wa kawaida. Hakuna urafiki wa kawaida
kati ya mtu na ex wake. Ukiona walishaachana lakini bado wanajifanya ni
marafiki wa kawaida, lazima ujue kwamba kuna mchezo unaochezeka nyuma ya
kisogo chako.
5.
Anakasirika akisikia ex wake anatoka na mtu mwingine. Hii ni dalili
nyingine muhimu, hata kama walishaachana siku nyingi zilizopita, kama
bado ana hisia juu ya mpenzi wake wa zamani, atajisikia wivu na
kukasirika akisikia anatoka na mtu mwingine. Ataonesha wivu waziwazi,
atamchukia, atamsema vibaya na wakati mwingine hata kupigana na mpenzi
mpya wa ex wake.
6. Anaendelea kumpa misaada mbalimbali. Ukiona mpenzi wako anaendelea
kumsaidia ex wake kama kumtumia muda wa maongezi, fedha za matumizi au
kodi ya chumba, ujue bado wanapendana na anafanya hayo kwa sababu
anaamini ipo siku watarudiana.
7. Bado anazo zawadi walizokuwa wanapeana kipindi cha nyuma. Ukiona
mpenzi wako bado anatunza zawadi walizowahi kupeana na ex wake kipindi
cha mapenzi yao, ni dhahiri kwamba bado anampenda na wanaendelea
kuwasiliana.
Yawezekana pia kwenye simu yake bado kuna sms au picha walizokuwa
wakitumiana kipindi cha nyuma, amezihifadhi hataki kuzifuta! Hiyo ni
dalili kwamba bado anampenda.
MBINU ZA KUKABILIANA NA TATIZO HILI
Kuna usemi wa wahenga kwamba ukishalijua tatizo ni rahisi sana kukabiliana nalo ndiyo maana kabla ya kukupa mbinu za kupambana na tatizo la mpenzi wako kuwasilianana ex wake, nimeanza kwa kukupa dalili ambazo ukiziona, ujue bado anampenda ex wake na wanaendelea kuwasiliana.

Wiki jayo tutahitimisha mada yetu kwa kuangalia mbinu za kukabiliana
na tatizo hili baada ya kuwa umeshapata uhakika kwamba mpenzi wako bado
anampenda ex wake na wanaendelea kuwasiliana.
Endelea kulike: www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com

Post a Comment