MARCIO MAXIMO KUMALIZA UBISHI WA KHAMIS KIIZA NA EMMANUEL OKWI AGOSTI 17
Kocha mkuu wa Yanga sc, Marcio Maximo (kushoto) akimuelekeza jambo mshambuliaji wa klabu hiyo, Jerryson John Tegete (kulia)
YANGA SC inatarajia kuanika
hadharani wachezaji watakaoitumikia klabu hiyo msimu ujao wa ligi kuu
soka Tanzania bara na michuano ya kombe la shirikisho na wale
watakaoachwa Agosti 17 mwaka huu.
Afisa habari wa Yanga sc, Baraka
Kizuguto amekaririwa na baadhi ya vyombo vya habari jioni ya leo akisema
kuwa zoezi la usajili linaendelea vizuri ambapo viongozi wa kamati ya
usajili wanashirikiana kwa karibu zaidi na benchi la ufundi chini ya
kocha mkuu, Mbrazil, Marcio Maximo.
“Mwalimu anaendelea kufanyia kazi
ripoti yake pamoja na kutaja wachezaji anaowahitaji. Siku itapofika
ambayo ni Agosti 17, mwalimu ataweka kila kitu hadharani,” alisema
Kizuguto.
Baada ya Maximo kuwasajili
wachezaji wawili kutoka Brazil, kiungo mshambuliaji Andrey Coutinho na
mshambuliaji Gleison Santos Santana ‘Jaja’, Yanga imefikisha wachezaji
sita wa kigeni.
Kwa mujibu wa sheria inayotumika
kwa wachezaji wa kigeni kwa sasa, kila klabu ya ligi kuu inatakiwa kuwa
na wachezaji wa kigeni wasiozidi watano, hivyo Yanga inatakiwa kumuacha
mmoja.
Kumekuwa na mjadala mzito wa nani
anaichwa hususani kwa Waganda wawili, Khamis Kiiza na Emmanuel Okwi,
lakini Kizuguto alisema kila kitu ni Agosti 17 mwaka huu.
“Kuna Mbuyu Twite, Khamis Kiiza,
Haruna Niyonzima na Emmanuel Okwi, wote hatima yao itajulikana Agosti
17, hapo itajulikana nani atabaki Yanga na nani ataondoka,” aliongoza
Kizuguto.

Post a Comment