EVANS AVEVA ATENGA MAMILIONI KUKAMILISHA UJENZI WA UWANJA WA MAZOEZI BUNJU DAR
Muonekano wa uwanja wa Simba sc uliopo eneo la Bunju jijini Dar es salaam
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
TANGU Simba sc ianzishwe miaka ya
1930’s haijawahi kulimika uwanja wake wa mazoezi wala uwanja wa mazoezi
ukilinganisha na Azam fc iliyoanza kushiriki ligi kuu Tanzania bara
kwa mara ya kwanza msimu wa 2008/2009
Hii ni historia mbaya kwa klabu
kubwa kama Simba ambayo wakati wa kuanzishwa kwake ilikuwa inaitwa
Queens, baadaye Eagles, Dar Sunderland na mwaka 1971 ilibadilishwa jina
na kuitwa Simba Sports Club.
Simba yenye historia kubwa ya
soka la Tanzania sasa ipo katika mchakato wa ujenzi wa uwanja wake,
lakini leo katika hotuba yake, Rais wa klabu hiyo, Evans Elieza Aveva
amewahakikishiwa wanachama wa Simba kuwa miezi michache ijayo, klabu
itamiliki uwanja wake wa mazoezi.
Uongozi wa Ismail Aden Rage
ulianza utekelezaji wa ujenzi wa uwanja wa mazoezi eneo ya Bunju jijini
Dar es salaam na sasa maendeleo ni mazuri ambapo nyasi zilizopandwa na
zinaendelea kuota.
Aveva alisema uongozi wake umetengeza zaidi ya shilingi milioni 600 ili kukamilisha ujenzi wa uwanja wa mazoezi.
Pia Simba ipo katika mpango wa
kujenga Hosteli za wachezaji ili kuepukana na gharama kubwa wanazotumia
kuwaweka wachezaji Hotelini.

Post a Comment