MICHAEL RICHARD WAMBURA NA WENGINE 72 WAFUKUZWA UANACHAMA SIMBA SC
KLABU ya Simba imefanya mkutano
mkuu wa wanachama leo hii katika ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi,
Osterbay jijini Dar es salaam kujadili masuala mbalimbali ya klabu hiyo.
Mkutano huo ni wa kwanza tangu
viongozi wapya chini ya Rais Evans Eliaza Aveva na makamu wake Geofrey
Nyange ‘Kaburu’ waingie madarakani juni 29 mwaka huu.
Agenda za mkutano huo zilitangazwa
jana na Agenda ya 11 ambayo ilihusu wanachama 72 waliosimamishwa
uanachama na kamati tendaji ilitegemewa kuwa ya vuta ni kuvute.
Kama ilivyotabiriwa jana, leo hii
agenda hiyo ilivuta hisia za wengi na mwisho wa siku taarifa kutoka
kwenye mkutano huo zinaeleza kuwa mkutano mkuu umeamua kuwafuta
uanachamama (kuwafukuzwa) wale wote walioipeleka Simba mahakamani.
Idadi ya wanachama 72 pamoja na aliyekuwa mgombea wa Urais wa klabu hiyo, Michael Richard Wambura wamefutwa na kufukuzwa kabisa.
Taarifa zinaarifu kuwa maamuzi hayo yamechukuliwa na wanachama zaidi ya 800 waliohudhuria mkutano huo.
Wambura aliipeleka Simba
mahakamani mwaka 2010 wakati wanachama wengine waliobaki waliipekea
klabu mahakama kuu kanda ya Dar es salaam wakitaka uchaguzi mkuu
uliofanyika juni 29 mwaka huu usimamishwe kwa madai kuwa katiba
ilikiukwa na kamati ya uchaguzi ya Simba chini ya mwenyekiti wake,
mwanasheria, Dkt. Damas Wambura, lakini chanzo kikubwa kilikuwa
kuenguliwa kwa Wambura.
Hata hivyo kabla ya ya kufikia
maamuzi ya leo, Rais wa Simba Evans Aveva aliwataka wanachama
waliosimamishwa kujitokeza kwake na kuwasilisha utetezi, lakini hakuna
mwanachama aliyefanya hivyo.
Post a Comment