CHADEMA YAKANUSHA KUHUSIKA NA KIFO CHA MWANGOSI...VIDEO IPO HAPA JIONEE
Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Chadema, John Mnyika, akizungumza na waandishi wa habari.
Baadhi ya viongozi wa Chadema kutoka kushoto ni Ofisa Habari, Tumaini Makene, Mbunge wa Ubungo Mh. John Mnyika, Ofisa Mwandamizi Mafunzo na Uendeshaji, Mohamed Mtoi, na mwenye gwanda ni Katibu Mtendaji, Ofisi ya Katibu Mkuu, Victor Kimesera.
Jengo la makao makuu ya Chadema yaliyoko Kinondoni, Dar.
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimekana
shutuma zilizoelekezewa kwao kuwa wanahusika na kifo cha aliyekuwa
mwandishi wa habari wa Channel Ten, Daudi Mwangosi.Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Chadema, Mhe. John Mnyika, ameeleza kuwa hawahusiki na mauaji hayo bali ni propaganda zinazoenezwa ili kuwasahaulisha wananchi juu ya suala la katiba linaloendelea.
Mnyika alieleza kuwa wanaoeneza habari hizo ni wale ambao wanataka kuizuia Chadema na Ukawa kwa ujumla kuendelea na harakati za kupigania katiba ya wananchi ikiwemo kufanyika maandamano ya kitaifa iwapo Rais Kikwete hataingilia kati kulisimamisha zoezi la katiba mpya.
(Picha na Gabriel Ng’osha/GPL)
Post a Comment