BONGO MOVIE KIMENUKA,MTITU AGOMA KUTUMIKA KISIASA
Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, 'Steve Nyerere'.
YAMETIMIA! Kundi lililojipatia umaarufu mkubwa la
wasanii na waigizaji la Bongo Movie Unity, limeanza kumeguka baada ya
Katibu wake, William Mtitu kujiuzulu nafasi hiyo, akimtuhumu kiongozi
wao kuwatumia kisiasa.
“Nimechoka kutumiwa kisiasa bila ridhaa
yangu, kisingizio Bongo muvi, hiyo kitu hakuna kama kuna mtu au chama
kinahitaji kututumia wasanii au kuitumia Bongo muvi basi unatakiwa uwazi
na si kumtumia mtu mmoja kwa manufaa yake mwenyewe,” alisema Mtitu
alipoulizwa kulikoni.
CHANZO GLOBAL PUBLISHERS

Post a Comment