ad

ad

Jina la Okwi larudishwa Kamati ya TFF

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limemlalamikia mwanafamilia wa soka mmoja kwa Kamati ya Maadili kutokana na udanganyifu alioufanya katika suala la usajili wa kiungo mshambuliaji wa Yanga, Emmanuel Okwi.
Tayari TFF imepata ufafanuzi kutoka Fifa kwamba Okwi anaweza kuendelea kuichezea Yanga, lakini TFF imeibuka tena na kudai Sabri Mtulla alilidanganya shirikisho hilo kuhusu usajili wa Mganda huyo.

Akizungumza Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, alisema Mtulla analalamikiwa na TFF kwa madai ya kuidanganya Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji kuwa hakukuwa na pingamizi lolote juu ya usajili wa Okwi huku akijua wazi kuwa jambo hilo si kweli.
“Kwa mujibu wa kanuni, malalamiko hayo yamefikishwa kwenye Kamati ya Maadili ambayo itachunguza ili kujiridhisha kama yana msingi au la. Ikibaini kuna kesi ndipo mlalamikiwa atafika mbele ya kamati hiyo,” alisema Wambura.

Hii ina maana kuwa jina la Okwi ambaye amekuwa akijadiliwa mara kwa mara limerudishwa tena kwenye kamati kujadiliwa, ingawa maamuzi yoyote hayataweza kumzuia kucheza.
Okwi anatarajiwa kuichezea Yanga mchezo wa kwanza wa ligi kuu Jumamosi ijayo dhidi ya Ruvu Shooting baada ya Fifa kuiruhusu TFF kumtumia.

Okwi alisajiliwa Etoile du Sahel ya Tunisia kutoka Simba kwa kitita cha dola 300,000 (zaidi ya milioni 480) fedha ambazo Simba hawajazipata lakini baada ya muda mfupi aliondoka klabu hapo na kujiunga na Villa ya

Uganda, ambayo ilimuuza kwenda Yanga na utata mkubwa ukazuka.
Wambura pia alisema wanafamilia wengine wanne wa soka ambao ni Riziki Majala, Army Sentimea, Oden Mbaga na Samwel Mpenzu nao wanalalamikiwa kughushi nyaraka ili kuhalalisha mtihani wao wa utimamu wa mwili wa waamuzi.
Powered by Blogger.