WASTARA ADAIWA KUTOKA NA MPENZI WA AUNTY LULU!
Staa wa filamu Bongo, Wastara Juma akiwa na muigizaji mwenzake 'Bond'.
BAADA ya kuachwa na mpenzi
wake wa siku nyingi Bond, ambaye kwa sasa anadaiwa kuwa na uhusiano wa
kimapenzi na mwigizaji wa filamu, Wastara Juma, Aunty Lulu amekubali
yaishe na sasa hana tena kinyongo nao.
Mwigizaji wa filamu Bongo, 'Aunty Lulu'.
“Mimi sina tena kinyongo na Wastara, vile
nilikuwa namfanyia tu vituko, lakini kwa sasa asiniogope wala asiwe na
wasiwasi na mimi, nimeshaachana na Bond japokuwa tulitoka mbali sana na
hakuna wanamke anayemjua kama mimi, siku ya harusi yao nitacheza mpaka
asubuhi,”alisema Aunty Lulu.
Alisema kwa sasa hana kinyongo na Wastara na amebariki uhusiano wao wa kimapenzi.
Endelea ku-like www.facebook.com/2jiachie

Post a Comment