ad

ad

TOROJO BAMIA (Winga teleza) - 19





“Shuuuukuuu aashiii, unajuaaa, Shuku unajuaaa. Shuku niliota kutu kupakwa shombo na MJ leo chuma kimapata msasa safishaaa mpenziii.”
Lily alilalama huku akiiachia nyonga izungumze na Shuku naye alikuwa amemisi maini ya Lily kwa muda mrefu  mwiko ulifanya kazi ya kuyageuza kwa mahiri mkubwa. Alijigeuzia atakavyo, mpaka wanakwenda mapumziko Lily alikuwa ndwembwendembwe.
Baada ya mpambano wa kukata na shoka Lily aliangua kilio kilichomshtua Shuku.
“Lily unalia nini?”
“Kwa nini ulinidanganya?”
“Kukudanganya kivipi?”
“Kwa nini hukuniambia ukweli mwanzo wa penzi letu?”
“Nilijua nitakukosa, Lily nilikuwa nakupenda sana.”
“Kwa hiyo sasa hivi unipendi?”
“Narudi mimi na wewe nani hampendi mwenzake?”
“Wewe.”
“Nani aliyemsaliti mwenzake?”
“Wewe.”
“Kwa nini?”
“Hakuniambia ukweli kitu kilichosababisha niyaamini maneno ya MJ.”
“Kwa nini ulimuamini?”
“Mitego niliyokutega ndiyo iliyokunasa, kwa hiyo yote aliyoniambia niliyaamini. Ona raha hizi nilizipoteza Shuku nazidi kukulaumu kunidanganya.”
“Sasa kama uliyaamini tatizo nini?”
“Nimegundua MJ si mkweli mgombanishi kupitia fedha zake. Shuku yote umesababisha wewe,” Lily aliendelea kumlaumu Shuku.
“Lakini uli...”
“Shuku usiseme lolote kila siku nitakulaumu wewe.”
“Basi yamekwisha.”
“Shuku unanipenda?”
“Zaidi ya kukupenda.”
“Naomba usinidanganye ili nami nidumu kwenye penzi lako. Mimi si mpenda fedha kama unavyodhani bali naogopa kudanganywa.”
“Nimekuelewa mpenzi wangu.”
“Kama umenielewa nipe haki yangu.”
Shuku hakuwa na hiyana kwani hata yeye aliumia kuachwa na Lily mwanamke ambaye kwake ndiye aliyekuwa chaguo la moyo wake. Kazi ikawa bandika bandua kila mmoja alitaka kuonyesha anajua mapenzi mpaka raha ikageuka karaha na kuamua kupumzika wakiwa hoi.
                          ***
Penzi lilirudi kwa kasi huku Lily akimganda Shuku kama luba ili kuhakikisha hampotezi. Baada ya muda Lily aliuza nyumba na kuhamia kwa Shuku kujipanga na ndoa yao. Kila kitu kilikwenda kama kilivyopangwa. Siku ilipofika ilifungwa harusi ya kifahari huku MJ akichangia kwa kiasi kikubwa na siku ya harusi aliitumia kuomba msamaha kwa maharusi.
Shuku hakuwa na hiyana na rafiki yake alimsamehe huku akimpa onyo akimfuata tena mkewe atamteremsha mshipa. MJ alimwambia rafiki yake kuwa kuoa kwake kumpa fundisho kubwa hivyo naye aliamua kumtafuta mwanamke mmoja na kufunga naye ndoa kuanza maisha mapya.
Mpaka sasa hivi maisha yanakwenda Shuku na Lily wana mtoto mmoja na mke wa MJ anakula maembe mabichi na mate yanamjaa mdomoni.
                            MWISHO   

No comments

Powered by Blogger.