Penniel Mungilwa ‘VJ
Penny’.
Chereko? Habari ya mjini ni kwamba aliyekuwa laazizi
wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Penniel Mungilwa ‘VJ
Penny’ anadaiwa kujipoza kidonda cha kumwagana na mpenzi wake huyo baada
ya kutupia pete ya uchumba kidoleni.
Penniel
Mwingilwa amepost kwenye Instagram picha inayoonesha mkono wake wa
kushoto ukiwa juu ya usukani wa gari ambao una pete katika kidole cha
chanda.
Penny ambaye ni mtangazaji wa Kipindi cha Genge cha EFM aliifanya
ishu hiyo wikiendi iliyopita ambapo mwanadada huyo alitupia picha
akiendesha gari huku kidoleni akiwa na pete hiyo ya uchumba
iliyoambatana na maneno yaliyosomeka: “Road trip…site here we come”
akimaanisha yupo njiani kuelekea saiti.
‘VJ Penny’ akiwa na Diamond kwenye picha ya pamoja.
Safu hii ilimcheki Penny ili kujua chochote juu ya pete hiyo lakini
hakupatikana hewani huku akiendelea kutumiwa pongezi za kumwaga.
Tusubiri!
Post a Comment