KIGAUNI CHA WOLPER CHAIBUA MINONG’ONO
MH! Kigauni kifupi alichotinga staa wa sinema za
Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe katika hafla ya chakula cha usiku
iliyoandaliwa na Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve
Nyerere’ kimeibua minong’ono watu kuhoji kulikoni akivae hivyo ndani ya
Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

“Unajua siku zote tunaambiwa sisi Bongo Movie hatuna heshima, siyo kweli, kuna watu wapo kwa ajili ya kutudhalilisha. Angalia Wolper alichovaa,” alisema mwigizaji mmoja ambaye hakutaka jina liandikwe gazetini. Alipoulizwa Wolper kuhusiana na madai hayo ya udhalilishaji, alijibu:
“Achana nao hao ni wanafiki tu kwani kuna mtu amekatazwa kuvaa kama hivi?”
Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe
Tukio hilo lilowastaajabisha wengi lilijiri wikiendi iliyopita katika
Mgahawa wa Great Wall uliopo Masaki, Dar ambapo asilimia kubwa ya
waalikwa katika hafla hiyo walisema hakikustaili hasa kwenye mwezi huu
wa toba.“Unajua siku zote tunaambiwa sisi Bongo Movie hatuna heshima, siyo kweli, kuna watu wapo kwa ajili ya kutudhalilisha. Angalia Wolper alichovaa,” alisema mwigizaji mmoja ambaye hakutaka jina liandikwe gazetini. Alipoulizwa Wolper kuhusiana na madai hayo ya udhalilishaji, alijibu:
“Achana nao hao ni wanafiki tu kwani kuna mtu amekatazwa kuvaa kama hivi?”

Post a Comment