ad

ad

HATIMAYE FELAINI ANYOA AFRO LAKE



 Mchezaji huyo wa miaka 26 ametupia picha kwenye mtandao wa facebook kuonyesha muonekano wake mpya.
MAROUANE Fellaini amelipiga mkasi afro lake katika maandalizi ya kujipanga kwa msimu mpya wa Ligi Kuu ya England huku ikihofiwa kuwa anaweza akapigwa bei Manchester United.

Pengine baada ya kuwa na msimu mbovu kwa klabu yake pamoja na timu ya taifa ya Ubelgiji, Fellaini anadhani muonekano wake mpya unaweza kumfanya ‘azaliwe’ upya kisoka.

Hata hivyo muonekano huu mpya wa Fellaini, sio wa kwanza, aliwahi kuwa na muonekano huo wakati akikipiga na Standard Liege ya Ubelgiji kati ya mwaka 2004- 2006.

No comments

Powered by Blogger.