ARSENAL HAKUNA RONGO RONGO, ALEXIS SANCHEZ ASAINI MKATABA WA MIAKA MINNE KUKIPIGA EMIRATES
ALEXIS Sanchez – mtu ambaye Arsenal inaamini anaweza akachangia kuwapa taji la Ligi Kuu ya England – amekamilisha usajili wake wa pauni milioni 30 kutoka Barcelona.
Supastaa huyo wa Chile ambaye amekatiza mapumziko yake ili kukamilisha usajili wake London, alifuzu vipimo vya afya na kusaini mkataba wa miaka minne – kukukiwa na nafasi ya kuongeza miezi 12 – pamoja na mshahara wa pauni 140,000 kwa wiki. Fungu hilo linamweka daraja moja na Mesut Ozil.

“Nina furaha sana kujiunga na Arsenal, klabu yenye meneja bora, kikosi maridadi, mashabiki bab kubwa duniani kote pamoja na stadium yenye hadhi kubwa,” alisema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25.
“Naangalia mbele kukutana na wachezaji wenzangu na kuichezea Arsenal kwenye Premier League na Champions League.
“Nitacheza kwa ubora wangu wote ndani ya Arsenal na nataka kuwafanya mashabiki wote wafurahi.
Usajili huo sasa unasafisha njia ya mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez kwenda Barcelona kuziba nafasi yake.
CREDIT: SALUTI 5.COM

Post a Comment