ad

ad

UGOMVI WA KAJALA, WEMA WABUNGE WAINGILIA KATI


Mambo bado mabaya! Ule ugomvi wa mashosti wawili nyota katika tasnia ya sinema
Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ na Kajala Masanja ‘K’, sasa umechanja mbuga
hadi kufika mjengoni, ambako inadaiwa kuwa baadhi ya wabunge wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, wameingilia kati ili kuumaliza.
Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ na Kajala Masanja ‘K’, wakiwa kwenye pozi enzi za ushosti wao.
Kwa mujibu wa chanzo makini, baada ya mvutano wao wa muda mrefu, wabunge hao
 walimwita Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na
kumuuliza kama ni kweli wawili hao hawaelewani.
Inadaiwa kuwa Steve alikiri kutokuwepo kwa maelewano kati ya wawili hao ambao awali
walikuwa ni marafiki pete na kidole.
Ilisemekana kwamba baada ya kuhakikishiwa kuwepo kwa ishu hiyo, baadhi ya wabunge
 hao, hasa wapenda michezo na sanaa, walimuagiza Steve kulifanyia kazi tatizo hilo haraka, akishindwa basi awapelekee ili wawakalishe chini.

“Walimwambia Steve kwamba ni kitendo cha aibu kwa mastaa wakubwa kama hao
kugombana, hiyo inawapunguzia heshima kwani hiki kilikuwa ni kipindi cha kushikamana
kwa umoja ili kuisogeza mbele tasnia yao badala ya kulumbana,” kilisema chanzo hicho
kikikataa kutaja majina ya wabunge hao na kutaka aulizwe Steve.
Gazeti hili liliwasiliana na Steve juu ya ukweli wa madai hayo, ambaye alikubali kuwa ni
kweli baadhi ya wabunge wamemtaka kumaliza bifu kati ya waigizaji hao maarufu
Bongo kwani nyuma yao kuna vijana wengi wanatamani kuwa kama wao.
Kajala Masanja.
Risasi Jumatano lilizungumza na mbunge wa Kinondoni  Idd Azan ambaye
alisema hata yeye atawaunga mkono wabunge watakaojitolea kuwasuluhisha mastaa hao.

No comments

Powered by Blogger.