ad

ad

HABARI KAMILI: KIFO CHA GWAMAKA MUHITIMU WA CHUO CHA UHASIBU ARUSHA


 Marehemu Gwamaka  Mwamakula.

KIJANA anayejulikana kwa jina la Gwamaka Mwamakula amefariki dunia katika ajali ya gari alipokuwa akitoka kijijini Manyara kwenda mjini Kateshi usiku wa kuamkia jana.
Marehemu aliyekuwa akifanya kazi katika jeshi la polisi mkoani Manyara, alipata ajali hiyo baada ya gari lake dogo alilokuwa akiliendesha kugongwa na lori aina ya Fuso ambapo baada ya kupelekwa hospitali  alifariki dunia jana.
Mwili wa marehemu ulitarajiwa kuagwa leo huko Kateshi na mwili wake utasafirishwa kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika Mbezi-Mwisho siku ya Jumamosi.
Mwamakula alihitimu chuo cha Chuo cha Uhasibu Arusha - IAA -- mwaka 2011 katika kozi ya Habari na Mawasiliano (Information Technology).  Kwa mawasiliano zaidi piga namba hii 0714542375
Mungu ailaze roho ya marehemu Pema Peponi. Amen!

No comments

Powered by Blogger.