TAHARIFA: GWAMAKA KUZIKWA MBEZI-MWISHO SIKU YA JUMAMOSI DAR
Marehemu Gwamaka Mwamakula.
Gwamaka Mwamakula amefariki dunia katika ajali ya gari alipokuwa akitoka kijijini Manyara kwenda mjini Kateshi usiku wa kuamkia juzi.
Marehemu aliyekuwa akifanya kazi katika jeshi la polisi mkoani Manyara, alipata ajali hiyo baada ya gari lake dogo alilokuwa akiliendesha kugongwa na lori aina ya Fuso ambapo baada ya kupelekwa hospitali kuvuja damu kwa ndani alifariki dunia juzi saa nne asubuhi.
Mwili wa marehemu uliagwa siku ya jana huko Kateshi na mwili wake ulisafirishwa kuja Dar es Salaam siku ya jana kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika Mbezi-Mwisho siku ya Jumamosi.
Mwamakula alihitimu chuo cha Chuo cha Uhasibu Arusha - IAA -- mwaka 2011 katika kozi ya Habari na Mawasiliano (Information Technology). Kwa mawasiliano zaidi piga namba hii 0714542375
Mungu ailaze roho ya marehemu Pema Peponi. Amen!
Post a Comment