Kavumbagu abariki ufungaji bora kwa Tambwe
STRAIKA wa kimataifa wa Yanga, Mrundi, Didier
Kavumbagu, ameikubali kasi ya mabao ya Mrundi mwenzake anayekipiga
Simba, Amissi Tambwe na kukiri kuwa msimu huu mshambuliaji huyo atatwaa
kiatu cha ufungaji bora wa ligi.
Tambwe amefikisha jumla ya mabao 17 akiwa ndiye kinara huku akiwa tayari ameshaifikia idadi ya mfungaji bora wa msimu uliopita, mchezaji kutoka Ivory Coast, Kipre Tchetche wa Azam FC.
Akizungumza Kavumbagu alisema kwa sasa Tambwe yupo juu kutokana na spidi aliyonayo na kuna kila dalili ya kutwaa kiatu hicho msimu huu.
Hata hivyo, Kavumbagu alikiri kukihitaji kiatu hicho ambapo alisema kama ikitokea Mungu akimsaidia na kufunga mabao mengi zaidi kwenye mechi zilizobaki, itakuwa vizuri lakini kwa sasa anaangalia jinsi gani ataisaidia timu yake kuibuka na ubingwa msimu huu kisha ufungaji bora utakuja baadaye.
“Hilo suala lipo wazi, Tambwe yupo vizuri msimu huu, anakifanya kile kinachotakiwa tena kwa spidi kubwa, nafikiri ufungaji bora safari hii unaweza ukatua kwake, ni halali kabisa kwa sababu anachokifanya kinaonekana na vizuri mtu anapofanya kitu kizuri kumpa haki yake kwa kumsifia,” alisema Kavumbagu.

Post a Comment