ad

ad

MAN MOYES YACHAPWA 2-0 UGIRIKI

MAMBO yamezidi kumuendea kombo kocha David Moyes baada ya kuambulia kipigo cha mabao 2-0 mjini Athens Ugiriki. Nyota wa Arsenal anayecheza kwa mkopo Olympiacos, Joel Campbell alifunga bao la pili dakika ya 55 katika ushindi huo dhidi Manchester United kwenye mchezo wa kwanza hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa.
Campbell hakuwahi kugusa mpira The Gunners tangu aliposajiliwa mwaka 2011, lakini usiku huu alionyesha kiwango cha juu akiwa na jezi ya Olympiacos.
Alejandro Dominguez aliwafungia wenyeji bao la kuongoza dakika ya 38 na sasa United inatakiwa ishinde 3-0 katika mchezo wa marudiano mjini Manchester ili kusonga mbele.
Katika mchezo mwingine, wenyeji Zenit wamefungwa mabao 4-2 na Borrussia Dortmund. Mabao ya Dortmund yemefungwa na Mkhitaryan, Reus na Lewandowski mawili, wakati ya Zenit yamefungwa na Shatov na Hulk.
Wa mkopo; Campbell akishangilia baada ya kuiangamiza Man United usiku huu 
Celebration: Dominguez (centre) wheels away with his team-mates after scoring the opener in Greece
Sherehe: Dominguez (katikati) akishangilia na wenzake baada ya kufunga bao la kwanza
50/50: Olympiacos' Leadro Salino (left) fights with United's Ashley Young
Mchezaji wa Olympiacos, Leadro Salino (kushoto) akigombea mpira na Ashley Young wa United
Not happy: Rooney discusses another matter with referee Gianluca Rocchi after the second goal
Wayne Rooney akilalamika kwa refa Gianluca Rocchi baada ya bao la pili 
Nowhere to be seen: United were outplayed in every area in Greece on Wednesday night
Wachezaji wa United wakisikitika uwanjani
Powered by Blogger.