JAHAZI WAFAFANUA KUTAMBULISHA NYIMBO MPYA MOROGORO
KUNDI la Jahazi Modern Taarab limefafanua ni kwa nini limeamua
kuuchagua mji wa Morogoro kama kituo chao cha kwanza cha kutambulishia
nyimbo zao mpya zitakazounda albam yao mpya ijayo.
Jahazi wanatagemewa kufanya onyesho maalum Morogoro kwa ajili ya
kuwaonyesha nyimbo mpya mashabiki wao Ijumaa ya tarehe 31 mwezi huu
ndani ya ukumbi wa Tanzanite Complex.
Kiongozi wa Jahazi Modern Taraab, Mohamed Mauji, jana alifanya
mahojiano na kipindi cha Sham Sham za Pwani cha ITV kinachoongozwa na
mtangazaji Hawa Hassan (kama wanavyoonekana pichani) ambapo msanii huyo
alitoa sababu kadhaa ni kwanini wameichagua Morogoro. Kipindi hicho
kitaruka hewani tena Jumamosi hii saa 11 jioni.
Mauji ambaye ni mcharazaji gitaa la solo, alisema miongoni mwa
sababu nyingi ni pamoja na kuwa mji wa Morogoro ni ngome yao kubwa
(ukiondoa Dar es Salaam) hivyo safari hii wameupa heshima ya kipekee.
Mara zote Jahazi imekuwa ikianza kutambulisha nyimbo mpya jijini Dar
es Salaam na baadaye kufuatiwa na uzinduzi na baada ya hapo ndipo
wanazipeleka nyimbo mpya mikoani.
Mauji pia katika mahojiano yake hayo alifichua mikakati yao mikubwa ya kukakabiliana na ushindani kwa mwaka huu wa 2014.
Mauji pia katika mahojiano yake hayo alifichua mikakati yao mikubwa ya kukakabiliana na ushindani kwa mwaka huu wa 2014.

Post a Comment