JALI ILIYOWAUA PAUL WALKER, ROGER RODAS ZATOLEWA
Mabaki ya gari aina ya Porsche baada ya kugonga mti Jumamosi iliyopita na kumwua yeye na Roger Rodas.
Paul Walker akipozi mbele ya kamera wakati wa kushuti filamu ya " Fast and Furious 5," huko Rome, Italia, mwaka 2011.
Wazima
moto na askari wakilidhibiti eneo la ajali, ikiwa ni pamoja na kuwazuia
marafiki na ndugu wasijitose kwenye moto wa mlipuko wa gari husika.
Eneo la ajali linavyoonekana likiwa limejaa moshi.
Wachunguzi
wakiwa eneo ambapo gari hilo lilianza kugonga nguzo ya umeme katika
Mtaa wa Hercules karibu na eneo la Kelly Johnson Parkway huko Valencia.
VIDEO kuhusu ajali iliyomwua mcheza sinema maarufu
Mmarekani Paul Walker (40) na Roger Rodas (38) wakati gari lao aina ya
Porsche Carrera GT lilipoacha njia na kugonga mti kabla ya kuwaka moto,
imetolewa na mmoja wa mashuhuda amesema tukio hilo ni ajali na
halikuhusiana na kitu chochote kingine.Ajali hiyo iliyomhusisha staa wa filamu ya Fast and Furious, ilitokea Jumamosi wiki iliyopita huko California, Marekani.
Ajali hiyo ilirekodiwa na video za usalama zilizokuwa juu ya jengo moja la karibu ambazo zilionyesha moshi mwingi ukipanda juu na baadaye kutokea mlipuko.
Mashuhuda mwingine ambaye ni dereva amesema kwamba Rodas na Walker walilichukua gari lao kwenda kulijaribu kwa vile walihisi lilikuwa na dosari na wala hawakuwa wakiliendesha kwa ajili ya burudani.
CHANZO NI DAILY MAIL

Post a Comment