Rais Kikwete amteua Engineer Felchesmi Mramba kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amemteua Engineer Felchesmi Mramba kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika
la Umeme Tanzania (TANESCO).
Taarifa
iliyotolewa Ikulu, Dar Es Salaam leo, Jumatatu, Desemba 2, 2013, na
Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Florens Turuka inasema kuwa uteuzi huo
umeanza leo hii.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
2 Desemba, 2013

Post a Comment