Bahanuzi arudi Bongo kama alivyoondoka
MSHAMBULIAJI wa Yanga, Said Bahanuzi amemaliza
majaribio yake ya wiki moja aliyokwenda kufanya nchini Malaysia katika
Klabu za Teregganu na T-Team ambapo amerejea nchini.
Bahanuzi
aliondoka nchini Alhamisi iliyopita kuelekea nchini humo kwenda kufanya
majaribio ya wiki moja kwa ajili ya kucheza soka la kulipwa.
Akizungumza Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto alisema Bahanuzi alifanya majaribio
katika timu mbili tofauti alipokuwa Malaysia katika timu za Teregganu na
T-Team.
“Bahanuzi amemaliza leo (Jumatano) majaribio na usiku
ataanza safari ya kurudi Tanzania kwa ajili ya kujiunga na wenzake mara
baada ya kuwasili. Timu zote hizo zipo nchini Malaysia zinashiriki
Super League lakini majibu ya majaribio bado sijayapata,” alisema
Baraka.
CREDIT: GPL
Post a Comment