Morocco atamba kuipaisha Oljoro
Kikosi cha JKT Oljoro.
Na Amisa MmbagaKOCHA wa JKT Oljoro, Hemed Morocco, amesema atahakikisha anakipika vilivyo kikosi chake na kuwa tishio kwenye mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.
Morocco amejiunga na Oljoro kwa mkataba wa mwaka mmoja mara baada ya ajira yake katika timu ya Coastal Union kufikia tamati hivi karibuni.
Morocco ambaye ameanza majukumu mapya katika timu hiyo inayoshika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi, amesema vijana wake wapo vizuri na maandalizi yanaendelea na hakuna mchezaji ambaye ni majeruhi mpaka sasa.
“Wachezaji wapo vizuri kwani nimekaa nao kwa muda wa wiki mbili sasa japo sijawajua vizuri wachezaji wote lakini wanaonyesha muelekeo mzuri na naamini watafanya vizuri.
“Natarajia kukibadilisha kikosi kwa lengo la kufanya vizuri zaidi kwani tulifanya vibaya katika mzunguko wa kwanza,” alisema Morocco ambaye timu yake ina pointi 10 katika mechi 13.

Post a Comment