SITTA: Tanzania haitambui maamuzi yanayofanywa na wanachama EAC.
Tanzania
imetoa msimamo juu ya jumuiya ya afrika mashariki na kusisitiza
haitatambua maamuzi yoyote yatakayojadiliwa na kuamuliwa na baadhi ya
nchi wanachama nje ya utaratibu wa jumuiya.
Akijibu
swali la mbunge wa Viti maalum mhe. RUKIA AHMED nini msimamo wa
serikali juu ya mambo yanayohusu jumuiya ya Afrika Mashariki kujadiliwa
nakutolewa uamuzi bila ya Tanzania kushiriki.
Waziri
wa Afrika Mashariki Mheshimiwa SAMWEL SITTA Amewataka wabunge na
watanzania kutambua Tanzania iko makini katika kufuatilia yanayojitokea
katika ndani ya nchi wanachama wa jumuiya ya afrika mashariki.
Akijibu
swali la Mmbunge wa Same mashariki mhe anne kilango malecela aliyehoji
kwa nini Tanzania imekaa kimya katika kuhukua maamuzi, mheshimiwa SITTA
amesema serikali haijakaa kimya kuna hatua inazichukua na kusisitiza
mamlaka kuu wamekumaliana kutokushiriki katika vikao vyote ambavyo nchi
nyingine tayari wanaagenda zao.
Post a Comment