MFANYABIASHARA APIGWA RISASI JIJINI ARUSHA
Eneo la TRA, jijini Arusha.
Mwanamke mfanyabiashara aitwaye Valieth Mathias amepigwa risasi ya
mkononi leo akiwa katika benki ya CRDB eneo la TRA, jijini Arusha baada
ya kutokea mabishano kati yake na polisi wa benki hiyo.Chanzo cha tukio hilo kinasema kwamba Valieth Mathias alifika maeneo CRDB na kupaki gari yake akitaka kuingia Bank lakini akaambiwa eneo hilo halifai kupaki gari, alipaki gari na kuingia Bank alipotoka alikuta gari lake limetolewa upepo na ndipo vurugu ilianzaa baina yake na polisi. Vurugu ilipokuwa kubwa mama huyo aliwaambia polisi kwamba wasimtishie bunduki hata yeye anayo na alipotaka kuitoa polisi wakampiga risasi.Valieth Mathias huyo ni muuzaji maarufu wa madini jijini arusha.Mama huyo amekimbizwa hospitali na yupo chumba cha upasuaji.
Post a Comment