SIMBA, KAGERA SUGAR KUUMANA ALHAMISI, MECHI YAO NA AZAM YAINGIZA MILIONI 64
Na Boniface Wambura, Ilala
LIGI Kuu ya Vodacom (VPL) itaingia katika Raundi ya 12 keshokutwa (Oktoba 31 mwaka huu kwa mechi kati ya Simba na Kagera Sugar itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.

Viingilio
katika mechi hiyo itakayooneshwa moja kwa moja na Azam Tv kupitia TBC 1
vitakuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 kwa VIP A.
Nayo Yanga itashuka uwanjani Novemba Mosi mwaka huu katika mechi nyingine ya ligi hiyo dhidi ya JKT Ruvu itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Novemba 2 mwaka huu kutakuwa na mechi nne; Mgambo Shooting na Coastal Union (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Tanzania Prisons na Oljoro JKT (Uwanja wa Sokoine, Mbeya), Azam na Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), na Mtibwa Sugar na Rhino Rangers (Uwanja wa Manungu, Morogoro).
Nayo Yanga itashuka uwanjani Novemba Mosi mwaka huu katika mechi nyingine ya ligi hiyo dhidi ya JKT Ruvu itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
![]() |
| Kikosi cha Simba SC kilichomenyana na Azam FC. |
Novemba 2 mwaka huu kutakuwa na mechi nne; Mgambo Shooting na Coastal Union (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Tanzania Prisons na Oljoro JKT (Uwanja wa Sokoine, Mbeya), Azam na Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), na Mtibwa Sugar na Rhino Rangers (Uwanja wa Manungu, Morogoro).
Raundi
hiyo itakamilika Novemba 3 mwaka huu kwa mechi moja ambapo Mbeya City
itakuwa mwenyeji wa Ashanti United kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya
Sokoine jijini Mbeya.
Mechi
za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo zitachezwa Novemba 6 na 7
mwaka huu. Novemba 6 ni JKT Ruvu vs Coastal Union, Ashani United vs
Simba, Kagera Sugar vs Mgambo Shooting, Rhino Rangers vs Tanzania
Prisons na Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar.
Novemba 7 mwaka huu, Azam itacheza na Mbeya City wakati Yanga itacheza na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wakati
huo huo; Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Azam
lililochezwa jana (Oktoba 28 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
limeingiza sh. 64,261,000.
Mashabiki
waliohudhuria mechi hiyo namba 76 iliyomalizika kwa Azam kuibuka na
ushindi wa mabao 2-1 walikuwa 10,728 ambapo viingilio vilikuwa sh.
5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.
Mgawo
wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; Kodi ya Ongezeko la Thamani
(VAT) sh. 9,802,525.42, gharama za kuchapa tiketi sh. 3,793,490 wakati
kila klabu ilipata sh. 14,946,170.45.
Wamiliki
wa uwanja walipata sh. 7,599,747.49, gharama za mchezo sh.
4,599,848.61, Bodi ya Ligi sh. 4,599,848.61, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira
wa Miguu (FDF) sh. 2,279,924.31, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar
es Salaam (DRFA) sh. 1,773,274.46.
CREDIT BIN ZUBEIRY

Post a Comment