ad

ad

SHOO YA FIESTA DAR BAADA YA KUBUMA... KUENDELEA SAA 9 ALASIRI LEO

 Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya, Juma Kassim 'Sir Nature' akifanya vitu vyake stejini katika usiku wa Serengeti Fiesta 2013 ndani ya Leaders Club.…
 Linah akikatika sndani ya Serengeti Fiesta 2013.
NA 2JIACHIE,DAR.
BAADA ya shoo ya Tamasha la Serengeti Fiesta 2013 jijini Dar kusimama kwa muda leo alfajiri mida ya saa kumi na robo  kwa hitilafu ya umeme, itandelea tena saa 9 alasiri leo katika Viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam bila kiingilio.
Mashabiki wengi waliokuwepo katika Viwanja vya Leaders walishangazwa na kukatika kwa umeme kuanzia mida hiyo na kupelekea watu kuondoka katika Viwanja vya Leaders wakiwa katika nyuso za huzuni.

Baada ya kukatika kwa Umeme watu waliweza kusubilia kwa muda wa masaa 2 wakiwa wamekaa chini katika viwanja hivyo.

Chanzo chetu mpaka kinaondoka katika Viwanja hivyo wasanii kadhaa walikuwa bado hawajapanda ni Abdul 'Diamond Platnumz' Davido kutoka Nigeria, Mohombi kutoka Sweden, Nay wa Mitego,na wengineo wengi.

Akizungumza na baadhi ya mashabiki wa tamasha hilo waliokuwepo viwanjani hapo baada ya hitilafu kurekebishwa, Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba alisema kuwa shoo itaendelea saa 9 na wasanii Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' Davido kutoka Nigeria, Mohombi kutoka Sweden, Nay wa Mitego na Bendi ya Twanga Pepeta watatoa burudani ya nguvu.

Aliongeza kuwa mashabiki wategemee 'sapraiz' kibao wakati wa shoo hiyo. Wasanii waliopiga shoo baada ya umeme kurudi katika hali yake ni pamoja na Kalapina, Chid Benz na Darasa japo mashabiki wengi walikuwa wameondoka viwanjani hapo.
Powered by Blogger.