Mwanamuziki wa Kizazi Kipya Profesa Jay akabidhiwa Barcode yake leo

Mwanamuziki
Profesor Jay akiwa na mfano wa hundi yenye Barcode ambazo amekabidhiwa
leo, Jay anakuwa mwanamuziki wa Pili kuchukua Barcode za Tanzania katika
sekta ya muziki wa Bongo Fleva nchini.
Mwenyekiti
wa Bodi ya GS1 Tanzania Bw. Elibariki Mmari (Mwenye Koti la suti)
akizungumza wakati wa halfa fupi ya kumkabidi Barcode mwanamuziki wa
Kizazi Kipya Profesa Jay katika makao makuu ya Ofisi hiyo TIRDO Msasani
jijini Dar Es Salaam, Kulia kwa Bw. Mmari ni Fatma Kange Saleh Afisa
Mtendaji Mkuu wa GS1 Tanzania na Nd. Pius Mikongoti Afisa Muandamizi
toka GS1 Tanzania na kushoto kwa Mwenyekiti ni Bw. Joseph Haule aka
Profesa Jay.
Mwenyekiti
wa Bodi ya GS1 Tanzania Ndugu Mmari akimkabidi mfano wa hundi yenye
Barcode kwa ajili ya CD na nyimbo za mwanamuziki Pfofesa Jay huku
wajumbe wa Bodi ya GS1 Tanzania wakishuhudia.
Wanamuziki
nchini wameaswa kuchangamkia fursa zilizopo kwa kujitangaza na kutanua
wigo wa mashabiki wao kwa kujiunga na huduma ya Barcode. Hayo yamesemwa
leo na mwanamuziki Profesa Jay alipokuwa akikabidhiwa Barcode za ajili
ya CD yake mpya itakayojulikana kama The Best of Professor Jay ambayo
itakuwa na mchanganyiko wa nyimbo zake ambazo zime heat tangu kuanza
kwake. “nimeamua kutoka kivingine na kwa sasa nataka kufanya vitu
kimataifa kwa kusambaza kazi zangu kwenye mitandao ili niwafikie watu
wengi zaidi” alisema Jay.
Akiongea
katika makabidhiano hayo Mwenyekiti wa Bodi ya GS1 Tanzania Bw.
Elibariki Mmari alisema kuwa ni wakati muafaka kwa wanamuziki wa Tanznia
kuanza kuuza kwenye mitandao ya kijamii na masoko ya kwenye mtandao
kama wanavyofaidi fursa hizo wanamuziki wengine. Bwana Mmari alisema
kuwa kwa kutumia fursa hizo wanamuziki hao wanaweza kuuza kwenye
mitandao ya kijamii kwa kupitia makampuni makubwa duniani kama CD Baby
ambalo lina mikataba na maduka yote makubwa ya kwenye mtandao kama
iTune, Facebook Music na mengine makubwa.
Aidha
Mwenyekiti Mmari alitanabaisha kuwa wanamuziki wa Tanzania hawawezi
kuingia kwenye chati kubwa kama za Billboard bila kuwa na utambulisho wa
ki electroniki wa Alama za Mistari yaani Barcode. Naye Afisa muandamizi
wa GS1 Tanzania Bw. Pius Mikongoti alisema kuwa ni vigumu kupata
takwimu sahihi za usambazaji za wanamuziki wa Tanzania kwani kazi zao
haziko kwenye mfumo rasmi, “ukiangalia mwanamuziki kama Lady Jay Dee
mathalani ana wafuasi wamefikia laki moja kwenye mtandao wake wa kijamii
wa Facebook kama atatangaza kuuza kazi zake kwenye mitandao hiyo ni
wazi atawafiukia washabiki wake kirahisi zaidi” Takwimu za Billboard
zinachukuliwa kutokana na usambazaji na mauzo ya kazi za mwanamuziki ki
electroniki, ni vigumu kwa mwanamuziki kama Diamond ambaye kwa sasa ana
mashabiki lukuki na kazi zake kupigwa kila kona kupata takwimu sahihi za
usambazaji wake.
Aidha
amewataka wadau wa muziki nchini kuacha kusambaza nyimbo mpya za
wanamuziki kwenye mitandao na kuwafanya watu waweze kuzipata bila
kuzitolea chochote (downloads), kwa kufanya hivyo tunawaumiza wanamuziki
na tunakuwa hatuwasaidiii aliongeza Bw. Mikongoti. GS1 Tanzania ndio
watoaji pekee wa huduma za BArcode kwa bidhaa zote za Tanzania,
ikumbukwe kuwa ili uweze kuuza kwenye Supermarket na masoko ya
mitandaoni ni lazima uwe na alama hizi za mistari yaani Barcode.
Post a Comment