Manchester Utd kumuuza Rooney kwa pesa kiduchu
KUNA wasiwasi kwamba Manchester United wako katika hatihati ya
kumpoteza staa wao, Wayne Rooney kwa kumuuza pesa kiduchu kutokana na
klabu hiyo kushindwa kuanzisha mazungumzo ya mkataba mpya na mchezaji
huyo.
Mkataba wa sasa wa Rooney anayelipwa kiasi cha
Pauni 220,000 kwa mwezi na Manchester United umebakiza miezi 20 tu na
kuanzia sasa bei ya Rooney inatazamiwa kushuka kadri miezi ya kumalizika
mkataba wake inavyokaribia.
Katika dirisha lililopita, Rooney alikaribia kuondoka kwenda Chelsea, lakini Man United iliweka ngumu kwa kukataa ofa za Pauni 30 milioni kutoka kwa Chelsea na Arsenal ambao pia walijaribu bahati yao.
Katika dirisha lililopita, Rooney alikaribia kuondoka kwenda Chelsea, lakini Man United iliweka ngumu kwa kukataa ofa za Pauni 30 milioni kutoka kwa Chelsea na Arsenal ambao pia walijaribu bahati yao.
Mazungumzo ya Rooney na Manchester United yanatazamiwa kuingia dosari zaidi wiki hii kutokana na uzinduzi wa kitabu cha kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson ambacho kinatazamiwa kufafanua jinsi Rooney alivyojaribu kuihama United mara mbili.
Awali, katika pambano la mwisho la Ferguson Old Trafford dhidi ya Swansea msimu uliopita, Ferguson aliwaeleza mashabiki hadharani jinsi staa huyo wa zamani wa Everton alivyomuomba kuhama.
Kocha Jose Mourinho bado anamuona Rooney kama mshambuliaji pekee wa kunyanyua morali ya safu ya ushambuliaji, huku Arsene Wenger akiendelea kuangalia uwezekano wa kumtwaa nyota huyo.

Post a Comment